JKCI kutoa matibabu bure kwa watakaofanya vizuri katika kampeni ya “Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo Wako”


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu kitabu cha mtindo bora wa Maisha wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza uliofanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yenye kaulimbiu “Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo Wako”.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wananchi waliofika katika viwanja vya Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya mazoezi ya  kutembea umbali wa Km. 5 wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza uliofanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yenye kaulimbiu “Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo Wako”.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na wananchi waliofika katika  viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kutembea umbali wa Km.5 wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza uliofanyika hivi karibuni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yenye kaulimbiu “Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo Wako”.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akifanya mazoezi ya kutembea umbali wa Km. 5 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni sehemu ya kuihamasisha jamii umuhimu wa kufanya mazoezi iliyoandalia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yenye kaulimbiu “Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo Wako”.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau waliofanya mazoezi ya kutembea umbali wa Km. 5 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza iliyoandalia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yenye kaulimbiu “Tembea na JKCI, Linda Afya ya Moyo Wako”.

*********************************************************************************************************************************************************************************************************************

TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeahidi kutoa matibabu bure kwa watu ambao wataungana na taasisi hiyo katika kampeni ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

 Katika kampeni hizo zinazohusisha matembezi ya kilometa tano ambayo itafanyika kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi program maalum itawekwa ili kuwaona watu walioshiriki katika matembezi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa matembezi hayo,Mkurugenzi wa JKCI ,Dk. Peter Kisenge alisema program hiyo itapatikana kupitia simu ya kiganjani ambapo mhusika ataweka kilometa atakazotembea.

"Tutaanzisha hiyo app tutaweza kugundua ukifanya vizuri na kuweka hizo kilometa Taasisi ya moyo itakupa huduma bure na kukuweka VIP kwasababu umefanya vizuri naomba wananchi wajihusishe,”alisisitiza.

Alieleza kuwa wameona waandae program hiyo  maalum ambayo inaitwa ‘Tembea na Jakaya Kikwete ,linda afya ya moyo yako’ ili kuhamasisha jamii watembee.

Dk. Kisenge alisema wanataka program hiyo ienee nchi nzima kwa  kuhamasisha mashirika ,shule,nyumba zote,kila familia waweze kufanya mazoezi  kwasababu wanapofanya mazoezi wanajilinda na magonjwa yasiyoambukiza hususan moyo.

Alibainisha kuwa Magonjwa ya moyo yanaongezeka kwa kasi na watu wengi wanapoteza maisha Duniani kote karibu  watu milioni 17 na sasa wameanza kuona hata vijana wameanza kupata magonjwa ya moyo.

“Tunaona hao vijana wanakuja na mshtuko wa ghafla wa moyo katika taasisi yetu tumeona tuungane na serikali yetu kwamba tuhakikishe  haya magonjwa ya moyo yanapungua nchini kwetu na kumaliza kwani haya magonjwa yanachangia vifo,kupoteza nguvu kazi ,vijana wanapoteza maisha,”alieleza.

Alifafanua kuwa utafiti umeonesha kuwa hapa Tanzania mwaka 2012 mambo hatarishi ni uvutaji wa sigara,matumizi ya tumbaku,kutofanya mazoezi ,lishe isiyozingatia ubora,ulaji wa vyakula vyenye wanga sana ,kula nyama kwa wingi na ulaji pombe uliokithiri.

“Lakini unapofanya mazoezi kwa asilimia 10 unaweza kijikinga na haya matatizo  ndio maana tunasisitiza kufanya mazoezi .

Dk.Kisenge alisema Taasisi  imepanga kutembea mikoa 15 kuwafata wananchi popote pale walipo ambapo hadi sasa  wameshapita mikoa ya Geita,Arusha,Mtwara na sasa madaktari wao wako Mkoani Lindi  kuelimisha na kuwapima wananchi.

“Kwa mwaka huu tumefanya upimaji wa moyo kwa watoto na watu wazima  kwa Dar es salaam,Pwani,Arusha,Geita,Mtwara na Lindi  tayari tumeona watu 3,935 waliofanyiwa  vipimo kati ya hao watu 1391  walikuwa na magonjwa mbalimbali ya moyo ikiwemo shikizo la damu ,kutanuka kwa misuli  ya moyo ,kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo,matundu ya moyo hasa kwa watoto,valvu za moyo zilizoharibika.

Aidha alieleza kuwa waliwapa rufaa Wagonjwa 335 kutibiwa Jkci kwani kuna watu waliwakuta wanatembea na presha za juu za  200/123 huku wakiwa hawajijui.

Alisema Sasa wanaanza kutoa elimu kwa nchi nyingine ambapo hivi karibuni watu wa Zambia walikuja hapa na wa Malawi waliwaomba waende kule  na nchi nyingi za Afrika wanataka kuja kuona nini kinafanyika.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa matembezi hayo ,Naibu wa Spika la Bunge la Tanzania, Mhe. Zungu Azani alisema Maambukizi ya VVU yameongezeka kwa asilimi 40 kwa vijana ambapo hiyo ni  hatari kwa taifa na kuwataka vijana kujaribu kuepuka ngono isiyo salama  na kujiingiza katika ulevi na kujikuta wanafanya mambo ambayo hayapendezi.

“Niwapongeze JKCI kwa namna walivyopambana kuanzisha zoezi hili na niwahakikishie itakuwa ya kwanza Tanzania,makundi yote ya jogging tutayaleta  tutakuwa watu sio chini ya 5000 watakuja kushiriki katika mtembezi .

Mhe. Zungu alisema katika ziara anayotaraji kufanya nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ataenda kutangaza huduma zinazopatikana JKCI.

“Kesho nakwenda Kinshasa kwa kazi maalum ya serikali lakini nimemuomba mkurugenzi anipatie vipeperushi vya hospitali hii ili wananchi ya Kinshasa badala ya kwenda nje waje kutibiwa hapa nchinI, hospitali kuna kipimo cha damu inapima kinatoa taarifa ya miaka mitano ijayo kama kutakuwa na madhara kwenye mwili wako nchi nyingi hawana,’alisisitiza.

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari