Posts

Showing posts from January, 2023

JKCI yaokoa milioni 951 matibabu ya wagonjwa 25 nje ya nchi

Image

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi aipongeza JKCI kwa ubunifu wa kutoa kinga na tiba ya maradhi ya moyo nchini

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt.Peter Kisenge, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Hassan Khamis Hafidh, baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Kuhamasisha Upimaji wa Moyo, Kufanya mazoezi “Tembea na JKCI Linda Afya ya Moyo Wako” na Ufungaji wa Kambi ya Upimaji wa Moyo iliyofanyika tarehe 23-27 Januari 2023 , katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Unguja Jijini Zanzibar. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Kuhamasisha Upimaji wa Moyo, Kufanya mazoezi “Tembea na JKCI Linda Afya ya Moyo Wako” na Ufungaji wa Kambi ya Upimaji wa Moyo iliyofanyika tarehe 23-27 Januari 2023 , katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Unguja Jijini Zanzibar. ***********

RAIS wa Zanzibar Dkt.Hussein Ali Mwinyi aongoza matembezi ya kuhamasisha upimaji na matibabu ya moyo

Image

Dkt.Mwinyi aongoza matembezi ya kuhamasisha upimaji wa moyo na kufanya mazoezi

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia na wananchi wa mitaa ya Muembemimba akiwa katika Matembezi ya Kuhamasisha Ufanyaji wa Mazoezi  “Tembea na JKCI Linda Afya ya Moyo Wako” na Kufunga Kambi ya Upimaji wa Moyo iliyofanyika katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Unguja Jijini Zanzibar kuazia 23 - 27, Januari 2023. Matembezi hayo yalianzia  katika viwanja vya Maisra Suleiman na kumalizikia katika Uwanja wa Amaan Unguja leo 28-1-2023. Kushoto kwa  Rais ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika Matembezi ya Kuhamasisha Ufanyaji wa Mazoezi  “Tembea na JKCI Linda Afya ya Moyo Wako” na Kufunga Kambi ya Upimaji wa Moyo iliyofanyika katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Unguja kuazia 23-27, Januari 2023, matembezi hayo yaliyoanzia katika viwanja vya Maisara Suleiman na kumalizikia katika Uwanja wa Amaan U

Watu 718 wafanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo Zanzibar

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kumalizika kwa kambi maalum ya matibabu na upimaji wa magonjwa ya moyo ya siku tano iliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar Dkt. Muhiddin Abdi Mahmoud. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kumalizika kwa kambi maalum ya matibabu na upimaji wa magonjwa ya moyo ya siku tano iliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar. Katika kambi hiyo jumla ya watu 718 walipata huduma za upimaji na matibabu ambapo 75 walipewa rufaa ya Kwenda  kutibiwa JKCI . Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar Dkt. Muhiddin Abdi Mahmoud akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kumalizika kwa kambi maalum ya matibabu na upimaji wa magonjwa ya moyo iliyofanyika katik

Idadi ya Wagonjwa wa moyo wanaotibiwa nchini India yapungua

Image
Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao kutoka Hospitali ya Max iliyopo nchini India Dkt. Viveka Kumar wakimfanyia upasuaji wa tundu dogo mgonjwa ambaye mfumo wake wa umeme wa moyo una hitilafu katika kambi maalum ya siku tatu iliyomalizika jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wagonjwa 13 wenye matatizo mbalimbali ya moyo wametibiwa katika kambi hiyo Picha na Khamis Mussa ********************************************************************************************************* Idadi ya wagonjwa wa moyo wanaotibiwa nchini India yapungua kutokana na uwepo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inayotoa matibabu ya kibingwa ya magonjwa hayo. Hali hiyo imejidhihirisha baada ya Taasisi hiyo kupokea wagonjwa ambao zamani walikuwa wakienda nchini India kwa ajili ya matibabu mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo. Akizungumza na waandishi wa habari mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalumu ya matibabu ya moyo

JKCI yaokoa milioni 951 matibabu ya wagonjwa 25 nje ya nchi

Image
Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na mwenzao kutoka Hospitali ya Max iliyopo nchini India Dkt. Sinha Kumar kuvuna mshipa wa damu katika mguu wa mgonjwa utakaopandikizwa katika moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa wagonjwa ambayo mioyo yao inafanya kazi kwa asilimia 17 hadi 45. Jumla ya wagonjwa 25 wamepatiwa matibabu katika kambi hiyo   Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na mwenzao kutoka Hospitali ya Max iliyopo nchini India Dkt. Sinha Kumar wakipandikiza mshipa wa damu katika moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa wagonjwa ambayo mioyo yao inafanya kazi kwa asilimia 17 hadi 45. Jumla ya wagonjwa 25 wamepatiwa matibabu katika kambi hiyo Picha na: Khamis Mussa **************************************************************************************************************** Taasisi

‘Muungano umeboresha upatikanaji wa huduma za afya’

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Mrisho akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alipomtembelea ofisini kwake leo kwa ajili ya kuona ni namna gani watashirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar katika kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa wananchi. K  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Dkt. Hassan Khamis Hafidh kitabu chenye maelezo ya Taasisi hiyo wakati mkurugenzi huyo alipomtembelea Katibu Mkuu wa wizara hiyo kwa ajili ya kuona ni namna gani JKCI itashirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar katika kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa wananchi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Mrisho na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar Dkt. Muhiddin Abdi Mahmoud. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Fatma Mrisho akisal

Siku ya tatu Zanzibar wananchi waendelea kupimwa na kutibiwa magonjwa ya moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimwelekeza leo mzee Farouk Tahir jinsi mishipa ya damu ya moyo inavyoziba pamoja na madhara ya kuziba kwa mishipa hiyo wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya siku tano  inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar. Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa huduma ya matibabu kwa wananchi wa Visiwa vya Zanzibar waliofika katika  Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa moyo katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu kwa watoto na watu wazima. Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Paskal Kondi akimfanyia kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiogram - ECG) mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya siku tano  inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jaka

Wakazi wa Zanzibar waishukuru Serikali kwa kuwapelekea huduma ya kibingwa ya matibabu ya moyo

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akimfanyia mgonjwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography - ECHO) leo wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya siku tano  inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar. Daktari wa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jackline Mathew akimfanyia mtoto kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography - ECHO) leo wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya siku tano  inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar. Afisa Muuguzi wa  Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar Amina Hassan akimpima urefu na uzito mtoto aliyefika katika hospitali hiyo leo kwa ajili ya kupata huduma ya  upimaji na matibabu ya moyo. Kulia ni mama wa mtoto Salma Ali.    Maafisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji na mwenzake wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar Salama Rashid wakitoa elimu ya jinsi ya kuand