Dkt. Kisenge: Fanyeni kazi kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo wakati akifungua mafunzo yaliyofanyika  leo katika ukumbi wa JKCI jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kituo cha kazi  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo elekezi kwa  wafanyakazi hao yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Daktari bingwa wa upasuaji Alex Msoka akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira ambao wamepangiwa kituo cha kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo elekezi kwa  wafanyakazi yaliyofanyika  leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. 


 Afisa Utumishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kelvin Manyanga akiwafundisha wajibu wa mtumishi wa umma wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Na: JKCI

********************************************************************************************************************************

Wafanyakazi wapya katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma pamoja na maadili ya kitabibu ikiwa ni pamoja na kuwahudumia  wagonjwa kwa kufuata miongozi ya utoaji wa huduma za afya.

 

Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Dkt. Peter Kisenge wakati akifungua mafunzo elekezi kwa  wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sektetariate ya Ajira na kupangiwa kituo cha kazi katika Taasisi hiyo.

 

 “Taasisi yetu imekuwa na hadhi ya kimataifa kwani hivi sasa inapokea wagonjwa kutoka ndani ya nchi pamoja na wagonjwa kutoka Afrika Mashariki na kati, hivyo kwa wadhifa huu naamini mtashirikiana na wafanyakazi mliowakuta kuendelea kuijenga Taasisi hii”,. 

 

“Nimatumaini yangu mtafanya kazi kwa bidii, kuwa na maadili kama ambavyo utumishi wa umma unavyotutaka kuwa na kuhakikisha hamuwi sehemu ya kuhamasisha rushwa ama kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa tunaowahudumia”, alisema Dkt. Kisenge.

 

Dkt. Kisenge alisema Menejiment ya Taasisi hiyo itahakikisha wafanyakazi hao wanapata maslahi kutokana na utendaji wao wa kazi hivyo kuwataka kufuata mienendo ya wafanyakazi waliowakuta kazini.


Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wapya wenzake Daktari bingwa wa upasuaji Alex Msoka ameishukuru Serikali kwa kutoa ajira kwa waajiriwa hao na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kwa kufuata miongozo yote ya Serikali katika kuwahudumia wananchi wanaohitaji huduma za matibabu.


“Kama daktari nipo tayari kufanya kazi muda wowote, nilikuwa na shauku ya kufanya upasuaji wa moyo kwani ni eneo ambalo kwa sasa linakuwa sana hapa nchini hivyo kwangu mimi naamini nimekuja sehemu sahihi”, alisema Dkt. Alex.

 

Naye Mkuu wa Kitengo cha Watoto wenye magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Sulende Khuboja aliwahimiza wafanyakazi hao  kufanya kazi kwa kupendana kwani mahali pa kazi ni sehemu ambayo wafanyakazi hutumia muda mwingi wa kuishi.

 

“Wito wangu kwenu, fanyeni kazi kwa kushirikiana na kupendana kwani unapokuwa katika Taasisi hii unakuwa mmoja wa wanafamilia wa Taasisi hivyo upendo ni sehemu ya maisha yetu”, alisema Dkt. Khuboja.

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari