Siku ya tatu Zanzibar wananchi waendelea kupimwa na kutibiwa magonjwa ya moyo

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimwelekeza leo mzee Farouk Tahir jinsi mishipa ya damu ya moyo inavyoziba pamoja na madhara ya kuziba kwa mishipa hiyo wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya siku tano  inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar.

Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa huduma ya matibabu kwa wananchi wa Visiwa vya Zanzibar waliofika katika  Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa moyo katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu kwa watoto na watu wazima.

Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Paskal Kondi akimfanyia kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiogram - ECG) mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya matibabu ya moyo ya siku tano  inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar.


Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari