Ubalozi wa China watembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angella Muhozya akimuonesha moja ya
chumba cha kulipia (VIP) Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa China
nchini Tanzania Chu Kun alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma
za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo
na mfumo wa umeme wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Yona Gandye
akielezea huduma zinazotolewa katika chumba cha upasuaji wa moyo wa bila
kufungua kifua (Cathlab) wakati Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa
china nchini Tanzania Chu Kun alipotembelea JKCI leo kwa ajili ya kuangalia
huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angella Muhozya akimuelezea huduma
zinazotolewa na Taasisi hiyo Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa
China nchini Tanzania Chu Kun alipotembelea JKCI leo kwa ajili ya kuangalia
huduma za matibabu ya moyo zinazotolwea na Taasisi hiyo leo jijini Dar es
Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angella Muhozya akiwa katika picha ya pamoja
na Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Chu
Kun alipotembelea JKCI leo kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolewa na
Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam
Picha na: JKCI
************************************************************************************************
Comments
Post a Comment