Wazibwa matundu ya moyo kwa kutumia mashine ya ECHO
Wataalamu wa Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing nchini China wakimfanyia mtoto upasuaji wa kuziba tundu lililopo kwenye moyo bila kufungua kifua kwa kutumia mashine ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO). Upasuaji huo umefanyika bila kutumia mashine za mionzi kwa watoto 5. Wataalamu wa Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing nchini China wakiangalia muonekano wa moyo wa mtoto katika mashine ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wakiendelea na upasuaji wa kuziba tundu lililopo kwenye moyo bila kufungua kifua kwa kutumia mashine hiyo jana jijini Dar es Salaam. Upasuaji huo umefanyika bila kutumia mashine za mionzi kwa watoto 5. Wataalamu wa Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing nchini China wakiandaa vifaa kwaajili ya kumfanyia mtoto upasuaji...