Wazibwa matundu ya moyo kwa kutumia mashine ya ECHO
Wataalamu wa Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing nchini China wakimfanyia mtoto upasuaji wa kuziba tundu lililopo kwenye moyo bila kufungua kifua kwa kutumia mashine ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO). Upasuaji huo umefanyika bila kutumia mashine za mionzi kwa watoto 5.
Wataalamu wa Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing nchini China wakiangalia muonekano wa moyo wa mtoto katika mashine ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wakiendelea na upasuaji wa kuziba tundu lililopo kwenye moyo bila kufungua kifua kwa kutumia mashine hiyo jana jijini Dar es Salaam. Upasuaji huo umefanyika bila kutumia mashine za mionzi kwa watoto 5.
Wataalamu wa Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na
wenzao kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing nchini China wakiandaa vifaa
kwaajili ya kumfanyia mtoto upasuaji wa moyo bila kufungua kifua kwa kutumia
mashine ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati
wa kambi maalumu ya siku moja iliyofanyika katika Taasisi hiyo jana jijini Dar
es Salaam. Upasuaji huo umefanyika bila kutumia mashine za mionzi kwa watoto 5.
Wataalamu wa Afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing nchini China wakimfanyia mtoto upasuaji wa kuziba tundu lililopo kwenye moyo bila kufungua kifua kwa kutumia mashine ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO). Upasuaji huo umefanyika bila kutumia mashine za mionzi kwa watoto 5.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing nchini
China Xiangbin Pan akimsalimia mtoto anayesubiri kuingia katika chumba cha
upasuaji mdogo wa moyo wakati wa kambi maalumu ya siku moja iliyofanywa na
wataalamu hao kwakushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kuziba matundu yaliyopo kwenye moyo kwa watoto bila ya kufungua kifua na
bila kutumia mashine za mionzi.
Na: JKCI
*************************************************************************************************************************
Watoto watano wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo yaani
matundu wamefanyiwa upasuaji mdogo wa moyo bila kufungua kifua kwa kutumia
mashine ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – Echo).
Upasuji huo umefanyika bila kutumia mashine zenye mionzo wakati
wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali
ya Fuwai iliyopo Beijing nchini China.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kambi hiyo jana
jijini Dar es Salaam daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eva
Wakuganda alisema upasuaji huo umekuwa na manufaa kwao kwani wameweza kupata
mafunzo ambayo yameonesha kuwa na urahisi wa kufanyika kwa upasuaji na kuzuia
matumizi ya mionzi.
Dkt. Eva alisema wataalamu wa JKCI wamepata mafunzo ya hatua
kwa hatua kufanya upasuaji huo unaoweza kufanyika na kuleta mafanikio kwa jamii
kutokana na uwezekano wake wa kufanyika hata nje ya chumba cha upasuaji.
“Upasuaji tulioufanya hapa kupitia kambi hii ni mradi mkubwa ambao
unategemewa kwenda hadi vijijini, ni upasuaji ambao unaweza kufanyika hata
katika mazingira magumu na kuleta matokeo chanya”, alisema Dkt. Eva
Dkt. Eva alisema mafunzo hayo yanahitajika zaidi hasa kwa
wataalamu wa upasuaji mdogo wa moyo kwa watoto ili waweze kuhama kutoka kutumia
mashine za mionzi hadi upasuaji bila mionzi hivyo yaendelee kutolewa mara kwa
mara kwani siku moja haitoshi.
Vaileth Mkono kutoka Shinyanga ambaye mtoto wake ana tundu
kwenye moyo aliwashukuru wataalamu wa JKCI na wenzao kutoka Fuwai Beijini China
kwa kumfanyia upasuaji wa moyo kwa kutumia teknolojia ya kisasa kufunga tundu
lililokuwepo kwenye moyo wa mtoto wake.
Vaileth alisema anajisikia furaha kuona mwanae amefanyiwa
upasuaji kwani daktari alimwambia baada ya upasuaji huo mtoto atapona kabisa na
kuendelea na shughuli zingine kama ambavyo watoto wasiokuwa na magonjwa hayo
wanavyofanya.
“Tatizo hili limemsumbua sana mwanangu na kumfanya kushindwa kujichanganya na wenzake kucheza hivyo kuwa
mpweke lakini pia limemsababishia asianze shule hadi leo”,
“Mwanangu alianza kuumwa tangu akiwa na umri wa miezi mitatu
lakini hatukujua shida hadi pale nilipoenda Hospitali ya Bugando ndio
wakaniambia ana shida ya moyo na kunipa rufaa kufika hapa JKCI kwaajili ya
matibabu”, alisema Vaileth
Naye Mkurugenzi Mkuu kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo
Beijing nchini China Prof. Xiangbin Pan alisema wameleta ujuzi wa kufanya
upasuaji huo hapa nchini kuwasaidia watoto wenye magonjwa ya moyo wanaohitaji
huduma hiyo kutoka maeneo ya nje ya
mjini.
“Tunasema kuwasaidia watoto wanaokaa nje ya mjini
tukimaanisha kuwa upasuaji huu unaweza kufanyika hata nje ya hospitali, hivyo
kuwasaidia watoto ambao hawawezi kufika hapa kwaajili ya huduma hii”, alisema
Prof. Pan
Prof. Pan alisema wataalamu kutoka Hospitali ya Fuwai
wataendelea kuwapa ujuzi wataalamu wa JKCI mara kwa mara kwa kuendesha kambi
maalumu za pamoja na wakati mwingine kuwapa fursa wataalamu wa JKCI kupata
mafunzo hayo nchini China.
Comments
Post a Comment