Tanzania yapaa matibabu ya moyo kimataifa
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe wakati wa uzinduzi
wa kliniki ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tawi la Oysterbay lililopo
Oyster plaza Haile Salassie barabara ya Ali Bin Said leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna
Faraji akimuelezea Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama huduma inayotolewa na
kitengo cha Lishe kwa wagonjwa wa moyo wakati wa uzinduzi wa kliniki mpya ya
Taasisi hiyo iliyopo Oysterbay leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza daktari
bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Smita Bhalia wakati wa uzinduzi
wa Kliniki ya Oysterba leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akiwajulia hali wagonjwa waliofika
kutibiwa katika kliniki ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tawi la Kawe alipotembelea
Kliniki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza mgonjwa aliyefika
kutibiwa katika kliniki ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tawi la Kawe alipotembelea
kliniki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na viongozi
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea duka la dawa lililopo
katika kliniki ya JKCI Kawe leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na mabalozi
mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na wadau wa afya wakati
wa uzinduzi wa kliniki ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo
Oysterbay leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akielezea mafanikio ya taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa
kliniki mpya ya taasisi hiyo iliyopo Oysterbay leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mabalozi na viongozi mbalimbali wakifuatilia
matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa uzinduzi wa kliniki ya Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Oysterbay leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati
wa uzinduzi wa kliniki ya JKCI iliyopo Oysterbay leo jijini Dar es Salaam.
Na: JKCI
**************************************************************************************************************
Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa yanayoongoza barani Afrika
katika kutoa huduma za matibabu ya kibingwa hususani matibabu ya moyo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati
wa ufunguzi wa Kliniki ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iliyopo Oyster plaza
Haile Salassie barabara ya Ali Bin Said leo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Muhagama alisema Serikali imeendelea kufanya jitihada za
uwekezaji katika sekta ya afya lengo likiwa kukabiliana na vifo vitokanavyo na
magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo.
“Kadiri siku zinavyozidi kwenda serikali imeendelea kuwekeza
kwenye vifaa tiba na vifaa vya uchunguzi lakini haijasahau kuendelea kuwekeza
kwenye ubingwa na ubobezi kwa wataalamu wetu ili tuweze kuendelea kutoa huduma
kwa wananchi wanaotuamini”,
Mhe. Mhagama alisema Kliniki ya Oystebay si tu itahudumia
wageni wanaotoka nje ya nchi lakini pia
ni eneo ambalo linaweza kufikika kirahisi na watanzania wanaoishi katika maeneo
haya.
“Leo nimeweza kutembelea pia kliniki ya JKCI iliyopo Kawe na
kukuta wananchi wengi wanapata huduma pale ambao wameishukuru sana Serikali kwa
kuwapunguzia adha ya kufuata huduma mbali”, alisema Mhe. Jenista
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt Peter Kisenge aliesema JKCI imetumia zaidi ya bilioni 2.2
kuwekeza katika kliniki ya Oysterbay na Kliniki ya Kawe.
Dkt. Kisenge alisema vifaa vilivyopo katika kliniki hizo ni
vya hali ya juu, pamoja na mashine ambazo zinatumia akili bandia kwa ajili ya
kugundua tatizo alilonalo mgonjwa
“Kliniki yetu inatoa huduma za matibabu kupitia huduma
mtandao (Tele consultation) ambapo hata kama ukiwa nje ya Tanzania unaweza
kupata huduma kutoka kwa daktari wetu yeyote”,
Moja ya vitu vikubwa ambavyo vinaweza kuitambulisha taaasisi
yetu kwa upekee ni pamoja na kufanya upasuaji wa kubadilisha valvu ya moyo bila
kufungua kifua (TAVI Procedure) huu ni utaalamu wa hali ya juu”, alisema Dkt.
Kisenge
Dkt. Kisenge alisema Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
inaenda kuikomboa Afrika katika masuala ya moyo kwani nchi za Zambia, Malawi,
Comoro na Kongo sasa zimeanza kuitumia kwaajili ya kuzijengea uwezo.
Comments
Post a Comment