JKCI yapongezwa kwa kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo barani Afrika
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nicole
Kanyawa akimwelezea huduma zinazotolewa na taasisi hiyo Msanii wa Muziki nchini
Mrisho Mpoto atembelea banda la Taasisi hiyo lililiokuwa katika mkutano wa nishati wa wakuu wa nchi za
Afrika jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Benjamini akimuelezea namna moyo unavyofanya kazi mshiriki wa mkutano wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika kutoka nchini Malawi alipotembelea banda la Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nicole Kanyawa akimuelezea namna taasisi hiyo inavyofanya utalii tiba mshiriki wa mkutano wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika kutoka nchini Djibouti alipotembelea banda la taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Daktari kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika Nelly Iteba akizungumza na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuhusu masuala ya tiba utalii alipotembelea banda la JKCI wakati wa mkutano wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika.
Na: JKCI
*****************************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imepongezwa kwa kuwa
moja ya taasisi zinazotoa huduma ya matibabu bingwa bobezi ya moyo katika bara
la Afrika na kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje ya bara la Afrika
kufuata huduma hizo.
Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni na washiriki wa mkutano
wa nishati wa wakuu wa nchi za Afrika uliomalizika hivi karibuni jijini Dar es
Salaam waliotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Akizungumza wakati alipotembelea banda hilo raia wa Djibouti Raclud Abdilz alisema moja ya kitu alichojifunza hapa nchini ni pamoja na uwepo
wa Taasisi hiyo ya kibingwa inayotoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo
kwa watu kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
“Nimefurahishwa na taarifa za taasisi hii kwani sikuwa
naifahamu, sasa waafrika tunaweza kupata huduma ndani ya bara letu na karibu na
nchi zetu tofauti na kuzifuata mbali na nchi zetu”, alisema Raclud.
Naye Salu Omari kutoka nchini Malawi aliipongeza Taasisi hiyo
kwakuwa na ushirikiano mzuri na nchi ya Malawi kwani sasa wananchi wa Malawi
wanapata huduma JKCI.
“Mmekuwa mkija nchini Malawi kutuletea huduma zenu, leo
nimefika hapa Tanzania na kuona ambavyo nchi yenu imewekeza katika matibabu
haya ya moyo”, alisema Salu.
Taasisi hiyo inapokea wagonjwa kutoka nchi za Somalia, Malawi, Kenya, Rwanda, Visiwa vya Comoro, Msumbiji, Nigeria, Siera Leone, Zimbabwe, Uganda, Zambia, Congo, Ethiopia, Burundi nan chi zingine za nje ya bara la Afrika zikiwemo za Armenia, China, Ujerumani, India, Norway, Ufaransa, Uingereza na Marekani.
Comments
Post a Comment