Mhe. Balozi Mpoki apongezwa kwa kazi nzuri JKCI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Ulisubisya Mpoki akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpa zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Ulisubisya Mpoki kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa JKCI wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. 

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa wameshikana mikono na kuimba wimbo wa mshikamano baina ya wafanyakazi hao wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Daktari bingwa wa usingizi JKCI ambaye sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Ulisubisya Mpoki jana jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Ulisubisya Mpoki wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya wanaofanya kazi katika Idara ya Upasuaji wa moyo wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi Mpoki iliyofanyika jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Picha na: JKCI

*************************************************************************************************************

 

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)