Wafamasia watakiwa kufanya kazi kwa kufuata mifumo na taratibu za Taasisi
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete Dkt. Tatizo Waane akimkabidhi zawadi mfamasia aliyemaliza mafunzo ya
miezi sita kwa vitendo (Internship) Moza Salimu wakati wa hafla fupi ya kuwaaga
wafamasia waliomaliza muda wa mafunzo na kuwakaribisha wafamasia wanaoanza
mafunzo kwa vitendo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete Dkt. Tatizo Waane akimpatia cheti mfamasia aliyemaliza mafunzo ya miezi
sita kwa vitendo (Internship) Farahani Nikuli wakati wa hafla fupi ya kuwaaga
wafamasia waliomaliza muda wa mafunzo na kuwakaribisha wafamasia wanaoanza
mafunzo kwa vitendo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete Dkt. Tatizo Waane akimpatia cheti mfamasia aliyemaliza mafunzo ya miezi
sita kwa vitendo (Internship) Edington Nkuba wakati wa hafla fupi ya kuwaaga
wafamasia waliomaliza muda wa mafunzo na kuwakaribisha wafamasia wanaoanza
mafunzo kwa vitendo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete Dkt. Tatizo Waane akimpatia cheti mfamasia aliyemaliza mafunzo ya miezi
sita kwa vitendo (Internship) Hamphrey Mmanga wakati wa hafla fupi ya kuwaaga
wafamasia waliomaliza muda wa mafunzo na kuwakaribisha wafamasia wanaoanza
mafunzo kwa vitendo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Dkt. Tatizo Waane akimpatia cheti mfamasia aliyemaliza mafunzo ya miezi sita kwa vitendo (Internship) Sanson Luhangija wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wafamasia waliomaliza muda wa mafunzo na kuwakaribisha wafamasia wanaoanza mafunzo kwa vitendo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa
JKCI kwa kuzungumza na wafamasia waliomaliza mafunzo kwa vitendo (Internship)
katika Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwakaribisha wafamasia
wanaoanza mafunzo kwa vitendo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar
es Salaam.
Wafamasia wanaomaliza muda wa mafunzo kwa vitendo (Internship) na wanaoanza mafunzo hayo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwakaribisha wafamasia wapya iliyofanyika ikifanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Na: JKCI
*******************************************************************************************************
Wafamasia wanaoanza mafunzo kwa vitendo (Internship) katika
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kutumie muda wao kujifunza na
kufuata mifumo na taratibu za taasisi hiyo katika kutekeleza majukumu yao.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo
Dkt. Tatizo Waane wakati akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo
katika hafla fupi ya kuwaaga na kuwakaribisha wafamasia wanaopata mafunzo kwa
vitendo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Waane alisema JKCI ni moja ya Taasisi za Umma inayotoa
huduma bobezi na za kibingwa kwa wananchi waliopo ndani na nje ya nchi hivyo
kuwataka wafamasia hao kutumia taaluma zao kutekeleza majukumu yao kwa kufuata
miongozo ya kitaaluma na kuwajali wagonjwa.
“Hapa ukiwa mvivu hapatakufaa kwasababu sisi hapa kliniki
zetu zipo kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa mbili usiku, hivyo wakati
kliniki zinaendelea huduma za famasi pia zinatakiwa kuwa wazi”, alisema Dkt.
Waane
Aidha Dkt. Waane amewapongeza wafamasia waliomaliza muda wa
mafunzo kwa vitendo kwa kuwa watiifu na kutekeleza majukumu yao ya kazi bila ya
kuwa na vikwazo.
“Naamini kwa miezi sita mliyokuwepo hapa mmejifunza vitu
vingi ambavyo vitaenda kuwasaidia huko muendako, Sisi tumewaona na hata leo
tukisikia kuna nafasi ya mfamasia tupo tayari kuwapa fursa hizo kwasababu
tunawajua”, alisema Dkt. Waane
Kwa upande wake mfamasia wa JKCI Buganda Leonard amewapongeza
wafamasia waliomaliza mafunzo yao kwa vitendo kwa kufanya kazi kwa bidii na
kuwa na moyo wa kujifunza.
Buganda alisema kwa kipindi chote cha miezi sita wafamasia
hao wamekuwa watiifu na kufuata yale waliyokuwa wakielekezwa huku wakiwa sehemu
ya kuleta mabadiliko katika Taasisi.
“Mnapomaliza muda wenu hapa na kwenda kutafuta kazi muende
mkiwa na taswira ya yale mliyokuwa mkiyafanya hapa JKCI na kuwa mabalozi wetu
wazuri kupitia yale mliyojifunza hapa”, alisema Buganda
Akitoa shukrani zake mfamasia aliyemaliza muda wa mafunzo kwa
vitendo (Internship) Edington Nkuba alisema miezi sita ya kuwa JKCI imewapa
mafunzo makubwa wafamasia hao kuweza kutambua magonjwa ya moyo na dawa
zinazopaswa kupewa wagonjwa hao.
Edington alisema kupitia kitengo cha kutengeneza dawa
wafamasia waliokuwa kwenye mafunzo wameweza kutengeneza dawa za moyo za watoto
wanaohitaji dozi ndogo kabisa.
“Ukituangalia tulivyokuja na leo tunavyoondoka ni vitu viwili
tofauti, tunaondoka na ujuzi wa hali ya juu kwani ukiacha masuala ya kada yetu
kama wafamasia pia tumejifunza namna ya kutunza stoo za dawa, masuala ya
kutafuta wazabuni wa dawa na namna ya kununua dawa, lakini pia tumejifunza
masuala ya uongozi”, alisema Edington.
Naye mfamasia anayeanza mafunzo kwa vitendo katika Taasisi
hiyo Nicodemus Madyedye alisema kwa kipindi cha mwaka mmoja anachotegemea kuwa
katika Taasisi hiyo amejipanga kujifunza na kuwa sehemu ya kuleta faraja kwa
wagonjwa.
“Sisi ni wafamasia wakwanza kupewa muda wa mafunzo kwa
vitendo kwa kipindi cha mwaka mmoja katika Taasisi ya hii ya Kibingwa,
tumejipanga kutekeleza majukumu yetu ya kila siku kama vile tulivyoelekezwa”,
Tutaitumikia taasisi hii vyema na kuwatumikia wananchi
wanaokuja kupata huduma katika taasisi lengo letu likiwa kujenga nchi yetu
katika kutoa huduma bora za matibabu ya moyo”, alisema Nicodemus
Comments
Post a Comment