JKCI kushirikiana na Chuo Kikuu cha Heart Center cha nchini Ujerumani kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Heart Center kilichopo Hamburg nchini Ujerumani ambaye pia ni daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto Dkt. Daniel Biermann mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ya kuona ni namna gani chuo hicho kitashirikiana na JKCI kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiagana na mwanamuziki Ben Pol aliyeambatana na Naibu Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Heart Center kilichopo Hamburg nchini Ujerumani Dkt. Daniel Biermann pamoja na Marie Biermann walipotembelea taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona namna ambavyo chuo hicho kitashirikiana na JKCI kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto.
Comments
Post a Comment