Wanawake, wajawazito na watoto 178 wapimwa moyo Arusha kwa siku tatu
Daktari bingwa wa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rose Chengo akimpima kipimo cha kusikiliza mapigo ya moyo wa mtoto aliyefika na mzazi wake katika viwanja vya TBA Kaloleni karibu na Mnara wa Mwenge mkabala na Makumbusho ya Taifa Arusha kwaajili ya kupata huduma za upimaji wa moyo. Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wataalamu wanawake wa Taasisi ya Moyo jakaya Kikwete (JKCI) wanatoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito na watoto.
Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Oltrumet iliyopo wilaya ya Arusha Yohana
Ngadu akizungumza na wananchi wa mkoa wa
Arusha waliofika katika viwanja vya TBA Kaloleni karibu na Mnara wa Mwenge
mkabala na Makumbusho ya Taifa Arusha kwaajili ya kupata huduma za
upimaji wa moyo zinazotolewa na wataalamu wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI).Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake taasisi hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha wanatoa huduma za tiba
mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services
kwa kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito na watoto.
Wakazi wa mkoa wa Arusha wakisubiri kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo zinazotolewa na wataalamu wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) katika maonesho ya maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya Wanawake yanayofanyika katika viwanja vya TBA Kaloleni karibu na Mnara wa Mwenge mkabala na Makumbusho ya Taifa Arusha. Upimaji huo unafanyika kwa wanawake, wajawazito na watoto.
**************************************************************************************************************************************************************************************
Wanawake, wajawazito na watoto 178 wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo katika zoezi la upimaji wa magonjwa hayo linalofanyika jijini Arusha katika maonesho ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake.
Upimaji huo wa siku nane unafanywa na wataalamu wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika viwanja vya TBA Kaloleni karibu na Mnara wa Mwenge mkabala na Makumbusho ya Taifa Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Arusha daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto na Mkuu wa Kitengo cha Utoaji wa Huduma Bora wa Taasisi hiyo Dkt. Naiz Majani alisema leo ni siku ya tatu tangu wameanza kufanya upimaji huo na wameona wanawake 88, wajawazito 42 na watoto 48.
Dkt. Naiz alisema katika upimaji huo
wamewapima wanawake wajawazito kipimo cha Echokadiografia ya moyo wa mtoto
aliyepo tumboni, kipimo hicho kinamsaidia mama kutambua afya ya moyo wa mtoto
wake kabla hajajifungua kwani ni muhimu kwa wajawazito kufanya uchunguzi wa afya ya
moyo wa mtoto awapo tumboni ili wataalamu wajue namna ya kutatua tatizo la
mtoto kama anashida katika hatua za awali.
Dkt. Naiz alisema katika matibabu ya maradhi ya moyo wanayotoa JKCI wamebaini magonjwa mengi ya moyo kwa watoto kama yangegundulika mapema watoto hao wangetibiwa mapema na kupona.
Willian Mute mkazi wa Kaloleni alisema alikuwa na tatizo la moyo kwenda mbio baada ya kufanyiwa vipimo vya katika hospitali ya Mount Meru alikutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu na kuanzishiwa dawa ila baada ya kusikia kuna wataalamu wa moyo wako jijini Arusha akaona atumie nafasi hiyo kupima tena afya ya moyo wake.
“Nashukuru sana nimepima afya ya moyo wa mtoto wangu aliyepo tumboni namshukuru Mungu yuko salama, nawaomba kinamama wenzangu ambao ni wajawazito watumie nafasi hii kupima na kutambua afya za mioyo ya watoto wao ili kama watakutwa na shida ya moyo waanze matibabu mapema mara baada ya kuzaliwa”, alishukuru Mariam Juma mkazi wa Mianzini.
Comments
Post a Comment