Wakazi wa Arusha wapata huduma za uchunguzi wa moyo
Daktari bingwa wa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rose Chengo akichuwa taarifa za mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja vya TBA Kaloleni Arusha kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa moyo. Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wataalamu wanawake wa Taasisi hiyo wanatoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito, watoto na wanaume waliojitokeza kupata huduma hiyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na Mkuu wa Kitengo cha Vipimo vya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Engerasia Kifai akizungumza na mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja vya TBA Kaloleni jijini Arusha kwa ajili ya kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo. Katika kudhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wataalamu wanawake wa taasisi hiyo wanafanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito, watoto na wanaume waliojitokeza kupata huduma hiyo.
Comments
Post a Comment