Madaktari bingwa wa moyo wanawake watoa huduma za uchunguzi wa moyo Arusha


Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto na Mkuu wa Kitengo Maalumu cha Utoaji wa Huduma Bora wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Naiz Majani akimpima mama mjamzito kipimo cha Echokadiografia ya moyo wa mtoto aliyepo tumboni wakati wa maonesho ya maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya Wanawake yanayofanyika kwenye viwanja vya TBA Kaloleni jijini Arusha. Wataalamu wanawake wa taasisi hiyo wanafanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito, watoto na wanaume waliojitokeza kupata huduma hiyo.



Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na Mkuu wa Kitengo cha Vipimo vya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Engerasia Kifai akizungumza na mkazi wa Arusha aliyefika katika viwanja  vya TBA Kaloleni jijini Arusha kwa ajili ya kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo. Katika kudhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wataalamu wanawake wa taasisi hiyo wanafanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito, watoto na wanaume waliojitokeza kupata huduma hiyo.



Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Evelyne Furumbe akimpima mtoto kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi katika maonesho ya maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya Wanawake yanayofanyika kwenye viwanja vya TBA Kaloleni jijini Arusha. Kushoto ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto na Mkuu wa Kitengo Maalumu cha Utoaji wa Huduma Bora wa Taasisi hiyo Dkt. Naiz Majani.



Daktari bingwa wa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rose Chengo akimpima kipimo cha kusikiliza mapigo ya moyo wa mtoto aliyefika na mzazi wake katika viwanja vya TBA Kaloleni  Arusha kwaajili ya kupata huduma za upimaji wa moyo. Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wataalamu wanawake wa Taasisi hiyo wanatoa huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanawake, wajawazito, watoto na wanaume waliojitokeza kupata huduma hiyo.


Wakazi wa mkoa wa Arusha wakisubiri kupata huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo zinazotolewa na wataalamu wanawake wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) katika maonesho ya maadhimisho ya Kimataifa ya siku ya Wanawake yanayofanyika kwenye viwanja vya TBA Kaloleni jijini Arusha. Jumla ya watu 301 wakiwemo wanawake, wajawazito, watoto na wanaume wamepata huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo.

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)