JKCI yapokea kifaa tiba cha upasuaji chenye thamani ya zaidi ya Tshs. milioni 50 kutoka GSM Foundation
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea kifaa
tiba (Sternal Saw) kinachotumika kufungua kifua wakati wa kufanya upasuaji
mkubwa wa moyo chenye thamani zaidi ya shilingi milioni 50 kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu wa GSM Foundation Faith Gugu wakati kampuni hiyo ilipotoa kifaa
hicho leo kwaajili ya kuimarisha huduma za matibabu ya moyo nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge
akimkabidhi Afisa Uuguzi wa JKCI katika Idara ya Upasuaji Hania Bwahama kifaa
tiba (Sternal Saw) kinachotumika kufungua kifua wakati wa kufanya upasuaji
mkubwa wa moyo chenye thamani zaidi ya shilingi milioni 50 kilichotolewa leo na
Kampuni ya GSM Foundation kwaajili ya kuimarisha huduma za matibabu ya moyo
nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea kifaa
tiba (Sternal Saw) kinachotumika kufungua kifua wakati wa kufanya upasuaji
mkubwa wa moyo chenye thamani zaidi ya shilingi milioni 50 kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu wa GSM Foundation Faith Gugu wakati kampuni hiyo ilipotoa kifaa
hicho leo kwaajili ya kuimarisha huduma za matibabu ya moyo nchini.
Na JKCI
************************************************************************************************************************************
Kampuni
ya GSM Foundation imeipatia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kifaa tiba
(Sternal Saw) kinachotumika kufungua kifua wakati wa kufanya upasuaji mkubwa wa
moyo chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea kifaa hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema kifaa hicho ni muhimu
katika utoaji wa huduma za upasuaji wa moyo kwa kuwa hutumika katika hatua za
awali za upasuaji wa kufungua kifua kabla ya kuendelea na hatua nyingine za
matibabu.
“Leo
tunafuraha kubwa kupokea kifaa tiba hiki kwa ajili ya upasuaji wa moyo. Kifaa
hiki kina mchango mkubwa katika kufanikisha upasuaji wa moyo na kimetolewa na
GSM Foundation wakati muafaka kwani Taasisi ina uhitaji wa kifaa hiki katika
kutoa huduma kwa wagonjwa wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo”, alisema Dkt.
Kisenge.
Dkt.
Kisenge alisema GSM Foundation imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kuunga
mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha sekta ya
afya nchini.
“Mwaka
huu GSM Foundation imewezesha utekelezaji wa huduma za tiba mkoba zinazotolewa
na Taasisi katika mikoa ya Arusha na Manyara hatua inayosaidia kusogeza huduma
bingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo karibu na wananchi. Aidha, mwaka 2025
GSM Foundation iliungana na wadau wengine kuwezesha upasuaji wa moyo kwa watoto
535 nchini”, alisema Dkt. Kisenge.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya GSM Foundation Faith Gugu alisema
JKCI imekuwa mshirika wao katika nyakati mbalimbali hivyo wakaona ni muhimu
kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo kwa kuipatia kifaa tiba hicho chenye
umuhimu mkubwa katika upasuaji wa moyo.
“Tunafahamu
kuwa JKCI ni Taasisi inayotambulika kwa kutoa huduma bingwa za matibabu ya moyo
Afrika Mashariki na Kati. Hivyo sisi kama GSM Foundation tukiwa sehemu ya wadau
wa sekta binafsi tumeona ni muhimu kushiriki katika kuunga mkono juhudi za
Serikali na kunufaika na uwekezaji uliofanyika katika Taasisi hii”, alisema
Faith.
Faith
alisema ushirikiano kati ya GSM Foundation na JKCI unalenga kuiwezesha Taasisi hiyo
kuendelea kutoa huduma bora za matibabu ya moyo na kuwafanya wananchi wapate
huduma hizo kwa urahisi zaidi.
“Tunaamini
kuwa kupitia ushirikiano wetu na JKCI tumechangia kuiwezesha Taasisi kuendelea
kutoa huduma bora za matibabu ya moyo na kuwawezesha wananchi kupata huduma
hizo kwa urahisi,” alisema Faith.
Naye
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika Idara ya Upasuaji
Hania Bwahama alisema kifaa tiba hicho hutumika katika upasuaji wa moyo
unaohusisha kufungua kifua kwa watoto na watu wazima.
“Kifaa
tiba hiki ni muhimu sana katika upasuaji wa moyo, tunawashukuru GSM Foundation
kwa kutupatia kifaa hiki kwani kitatusaidia kuboresha ufanisi katika utoaji wa
huduma bingwa za matibabu ya moyo”, alisema Hania.



Comments
Post a Comment