Posts

Showing posts from July, 2021

Mtambo mpya wa cathlab na carto 3 kuokoa maisha ya wagonjwa wenye hitila...

Image

Menejimenti ya JKCI yapokea kombe la mshindi wa kwanza kwa utoaji wa huduma za afya na matumizi ya Teknolojia katika tiba lililotolewa na TanTrade wakati wa Maonesho ya 45 ya Sabasaba

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wawakilishi wa JKCI walioshiriki Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yaliyomalizika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa kukabidhi kombe la mshindi wa kwanza kwa utoaji wa huduma za afya na matumizi ya Teknolojia katika tiba leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam  Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Agnes Kuhenga akitoa neno la pongezi kwa wawakilishi wa JKCI walioshiriki Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yaliyomalizika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa kukabidhi kombe la mshindi wa kwanza kwa utoaji wa huduma za afya na matumizi ya Teknolojia katika tiba leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam  Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Aloyce akitoa taarifa ya upimaji...

Taarifa kuhusu Chanjo dhidi ya ugonjwa wa korona

Image
 

Serikali yaombwa kutoa uelewa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ukiwemo ugonjwa wa moyo kwa wananchi

Image
Mkurugenzi wa Kurugenzi  ya Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akimpa kitabu cha jinsi ya kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza  mwananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo  kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yaliyomalizika hivi karibuni  katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa. Serikali imeombwa kutoa uelewa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo magonjwa ya   moyo kupitia vyombo   vya habari, makongamano na   mikutano ya hadhara kwa kufanya hivyo watu wengi wataepukana na magonjwa hayo. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya upimaji wa magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya   45 ya kimataifa ya Dar es Salaam   yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere...

Wahudumu wa afya nchini watakiwa kuwa wakarimu wakati wanawahudumia wateja na wagonjwa katika vituo vyao vya kazi – Dkt. Gwajima

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akizungumza na wajumbe wa timu ya kuratibu hatua za Tanzania kuelekea kwenye  Utalii tiba wakati wa uzinduzi wa timu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam. Wahudumu  wa afya nchini wametakiwa kuwa wakarimu wakati wanapowahudumia wateja na wagonjwa kwani  kufanya hivyo wataongeza idadi ya watumiaji wa huduma watakaokwenda kutibiwa katika vituo vyao na kuvutiwa wajiunge na bima za afya na hivyo kuongeza mapato ya vituo husika na kupitia kuvutia wateja wa kimataifa watainua uchumi wa nchi kwa ujumla wake. Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima wakati akizindua timu ya kuratibu hatua za Tanzania kuelekea  kwenye utalii wa tiba katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Waziri Dkt. Gwajima alisema asili ya bi...

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yapongezwa kwa kuanzisha duka la kuuza dawa za magonjwa mbalimbali ya binadamu

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Doroth Gwajima akisafisha mikono kwa kutumia kitakasa mikono kilichotengenezwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Compounding unit alipotembelea duka la dawa za magonjwa mbalimbali lililoanzishwa na Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa JKCI Dkt. Delilah Kimambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima ameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuanzisha duka la dawa linalouza   dawa za kutibu magonjwa   mbalimbali na kuzitaka Hospitali zingine kuiga mfano huo. Waziri Dkt. Gwajima amezitoa pongezi hizo  leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua maktaba ya watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo na saratani wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Dkt. Gwajima alisema kuwepo kwa duka hilo la dawa kutawasaidia wagonjwa wanaotibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbil...

Warembo wa Miss Tanzania wakabidhi maktaba ya watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo na saratani

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Doroth Gwajima akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Fr’ederic Clavier na mwanzilishi wa Taasisi ya Beauty Legacy Miss Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi kabla ya kuzindua maktaba ya watoto wanaolazwa hospitali kwa muda mrefu wakati wa uzinduzi wa maktaba hiyo uliofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo Jijini Dar es Salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameziomba sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kujenga maktaba za watoto katika Hospitali na vituo vya Umma vya kulelea watoto ili kuwasaidia kujenga afya ya akili kwa kujisomea, na kuwajenga kisaikolojia wakati wakipatiwa matibabu ya muda mrefu. Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua maktaba ya watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya Moyo na saratani wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa ...

Jengeni tabia ya kupima afya za mioyo yenu mara kwa mara - Prof. Janabi

Image
Wananchi wakipata huduma   ya ushauri wa magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wananchi wameshauriwa   kujenga mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara   ili   kufahamu kama wana magonjwa ya moyo   au la na kama wanamatatizo   wataweza   kupata matiba mapema kabla ya tatizo kuwa kubwa na kama hawana itawasaidia kujikinga ili   wasipate magonjwa hayo. Rai hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza na waandishi wa habari   katika maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Dar es Salaama (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa. Prof. Janabi alisema ni muhimu kwa wananchi kutumia maonesho hayo kupima afya zao na kupata uelewa wa jinsi ya kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo moyo, figo na saratani. “Katika banda letu tunapima vipimo mbalimbali vya magonjwa ya   moyo vik...

Huduma za ushauri, upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo zatolewa kwenye banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika maonesho ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa ushauri wa jinsi ya kuepuka magonjwa ya moyo kwa  mwananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo kwa ajili ya kupimwa magonjwa hayo wakati wa maonesho ya 45 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa. Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimwonesha kifaa kisaidizi cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri   (Pacemaker) mwananchi aliyetembelea   banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwahudumia wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya 45 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa. Wafamasia wa kampuni ya kuagiza na ku...