Wananchi wajitokeza kupima afya zao katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakati wa maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa.
Mteknolojia wa Maabara wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jordan Megabe akitoa elimu kuhusu
magonjwa ya moyo kwa mwananchi aliyetembelea banda la JKCI lililopo katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara
ya Kilwa Jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kupata huduma za vipimo vya magonjwa ya moyo
zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Martha Emmanuel akimpima urefu, uzito na uwiano wa urefu na uzito mwananchi
aliyetembelea banda la JKCI leo lililopo katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata
huduma za vipimo vya magonjwa ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina
Kazaura akitoa ushauri wa afya ya moyo
kwa mwananchi aliyetembelea banda la JKCI lililopo
katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa
Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma za vipimo vya magonjwa ya moyo
zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Joyce Kaiza akimpima shinikizo la damu (BP)mwananchi aliyetembelea
banda la JKCI leo lililopo katika viwanja vya
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo katika barabara ya Kilwa Jijini Dar
es Salaam kwa ajili ya kupata huduma za vipimo vya magonjwa ya moyo
zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Maria Samlongo akitoa ushauri wa ulaji unaofaa kwa mwananchi aliyetembelea
banda la JKCI leo lililopo katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo
katika barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma za
vipimo vya magonjwa ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Baraka Ndelwa akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo
unavyofanya kazi (Echocardiography) kwa kutumia mashine ya V-Scan mwananchi aliyetembelea
banda la JKCI lililopo katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo
katika barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma za
vipimo vya magonjwa ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Sophia Bishashara akimpima wingi wa sukari mwilini mwananchi aliyetembelea
banda la JKCI leo lililopo katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo katika barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma za vipimo vya
magonjwa ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Baadhi ya washiriki wa maonesho
ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa.
Comments
Post a Comment