Huduma za ushauri, upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo zatolewa kwenye banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika maonesho ya Sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam


 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa ushauri wa jinsi ya kuepuka magonjwa ya moyo kwa  mwananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo kwa ajili ya kupimwa magonjwa hayo wakati wa maonesho ya 45 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa.

Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimwonesha kifaa kisaidizi cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri  (Pacemaker) mwananchi aliyetembelea  banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwahudumia wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya 45 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa.

Wafamasia wa kampuni ya kuagiza na kusambaza dawa za binadamu ya Salama Pharmaceuticals Limited wakimpatia dawa za moyo bila malipo yoyote yale mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo.

Mteknolojia wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jordan Megabe akimchukuwa vipimo vya damu mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupimwa vipimo vya magonjwa ya moyo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimsikiliza Mfamasia wa kampuni ya kuagiza na kusambaza dawa za binadamu ya Salama Pharmaceuticals Limited Maila Kazoya alipokuwa akimweleza  aina za dawa wanazozitoa bila malipo kwa wananchi wanaokutwa  na matatizo ya moyo mara baada ya kupimwa na kukutwa na matatizo hayo na wataalamu wa JKCI.

Baadhi ya washiriki wa maonesho ya 45 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na  Julius Charles aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.


Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimpima urefu na uzito Julius Charles aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa wakati wa maonesho ya 45 ya Kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa.


Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)