Posts

Showing posts from September, 2021

JKCI yatoa huduma za vipimo vya magonjwa ya moyo katika mkutano wa mwaka wa madaktari

Image
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tatizo Waane akielezea huduma zinazotolewa na JKCI wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel alipotembelea banda la JKCI wakati wa Mkutano wa siku mbili wa madaktari uliofanyika katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akitoa taarifa ya upimaji uliofanyika katika Mkoa wa Geita wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel alipotembelea banda la JKCI wakati wa Mkutano wa siku mbili wa madaktari uliofanyika katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi wa Mkoa wa Mwanza aliyetembelea katika banda la JKCI wakati wa mkutano wa siku mbili wa madaktari uliofanyika katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tatizo Waane

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya wilaya ya Kigamboni waadhimisha siku ya Moyo Duniani kwa kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo kwa wananchi

Image
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akizingumza na wananchi waliofika katika viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Kigamboni iliyopo eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo uliofanywa na wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kigamboni ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani. Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kigamboni wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo Fatma Nyangasa wakati akizungumza nao kuhusu umuhimu wa kupima afya wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo bila malipo uliofanyika katika viwanja vya Hospitali ya wilaya ya Kigamboni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa akimsikiliza Alex Kyando kutoka kampuni ya uagizaji na usambazaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba ya Ajanta Pharma Limited alipokuwa akimweleza kuhusu aina ya dawa za moyo wanazozitoa  kwa watu waliokutwa na matatizo ya moyo wakati w

Wananchi Mkoa wa Geita wajitokeza kuchunguza magonjwa ya moyo

Image
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi wa Mkoa wa Geita aliyetembelea katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) jana katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bruno Selege akimpima kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) mwananchi wa Mkoa wa Geita aliyetembelea katika banda la JKCI kwa ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) jana katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akishirikiana na Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando Julieth Kabiligi kumfanyia uchunguzi mto

Katika kuadhimisha Siku ya Moyo Duniani tarehe 29/09/2021 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Wilaya ya Kigamboni watafanya upimaji wa magonjwa ya Moyo bila malipo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani.

Image
  Daktari  bingwa wa magonjwa ya moyo Baraka Ndelwa akimpima mwananchi kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiogram -ECHO).    

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yatoa elimu ya chanjo kwa wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)

Image
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akitoa elimu kuhusu chanjo ya UVIKO – 19 kwa wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) (hawapo pichani) wakati wataalam wa afya kutoka JKCI walipoalikwa na uongozi wa Benki hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo pamoja na kutoa chanjo kwa wafanyakazi hao jana katika viwanja vya benki hiyo vilivyopo Jijini Dar es Salaam. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.  Rashid Mfaume akielezea changamoto mbalimbali zinazotokana na ugonjwa wa UVIKO – 19 wakati wataalam wa afya kutoka JKCI walipoalikwa na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)   kwa ajili ya kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo pamoja na kutoa chanjo kwa wafanyakazi   hao jana katika viwanja vya benki hiyo vilivyopo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege akielezea namna ambavyo ameshawishika kuchanja chanjo ya UVIKO – 19 baada ya kupata elimu ku

Wanafunzi wanaosoma katika vyuo Vikuu nje ya nchi wapewa elimu ya Chanjo ya Uviko – 19

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa elimu ya Chanjo ya Uviko – 19 kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo Vikuu nje ya nchi kupitia Taasisi ya Global Education Link leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa elimu ya Chanjo ya Uviko – 19 kwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo Vikuu nje ya nchi kupitia Taasisi ya Global Education Link (hawapo pichani) leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam Wanafunzi wanaosoma katika vyuo Vikuu nje ya nchi kupitia Taasisi ya Global Education Link wakisikiliza wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) akitoa elimu ya chanjo ya Uviko – 19 leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.  

Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba wapimwa afya ya magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni maandalizi ya kushiriki mashindano ya ligi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika.

Image
Baadhi ya wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba wakisubiri kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wachezaji 32 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa magonjwa ya moyo kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya ligi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika.  Fundi sanifu wa moyo (Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Paschal Kondi akimpima kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba Rally Bwalya wakati wachezaji 32 wa timu hiyo walipofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya ya moyo kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya ligi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dickson Minja akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiog

Wagonjwa 9 wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo kwenye kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

Image
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu Subhash Sinha kutoka hospitali ya Max iliyopo New Delhi nchini India akishirikiana na madaktari bingwa wa upasuaji mkubwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupandikiza mishipa ya damu ya moyo (Coronary Artery Bypass Graft Surgery - CABG)  kwa mgonjwa bila ya kuusimamisha moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu inayofanyika katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam.  

Wafanyakazi wa Benki ya Exim Idara ya Fedha wachangia gharama za matibabu ya mtoto mwenye matatizo ya moyo

Image
Msimamizi wa Wodi ya Watoto ambaye pia ni Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theresia Marombe akiwaeleza wafanyakazi wa Benki ya Exim Idara ya Fedha waliofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuchangia gharama za upasuaji wa moyo kwa mtoto alizaliwa na   tundu kwenye moyo huduma zinazotolewa kwa wagonjwa wanaolazwa katika wodi hiyo. Mkuu wa Idara ya Fedha kutoka Benki ya  Exim Issa Hamisi akimkabidhi Mhasibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Isimbula kiasi cha Tshs. 3,000,000/= fedha zilizochangwa na  baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo  Idara ya Fedha kwa ajili ya kulipia gharama za upasuaji wa moyo kwa mtoto aliyezaliwa na tatizo la tundu kwenye moyo. Mama ambaye mtoto wake amezaliwa na tundu kwenye moyo Elizabeth John akipokea kiasi cha Tshs. 400,000/= kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya  Exim Issa Hamisi fedha ambazo atazitumia kwa ajili ya kununua chakula na mahitaji mengine  ya mtoto kabla na baada ya kufanyiwa upasuajia wa moyo utakaof