Wananchi Mkoa wa Geita wajitokeza kuchunguza magonjwa ya moyo


Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi wa Mkoa wa Geita aliyetembelea katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) jana katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita.


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bruno Selege akimpima kipimo cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) mwananchi wa Mkoa wa Geita aliyetembelea katika banda la JKCI kwa ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) jana katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita.


Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akishirikiana na Daktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando Julieth Kabiligi kumfanyia uchunguzi mtoto aliyebainika kuwa na presha ya juu kwenye mapafu pamoja na kutanuka kwa kuta za upande wa kulia wa moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) jana katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita.

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akimpima shinikizo la damu (BP) mwananchi wa mkoa wa Geita aliyetembelea banda la JKCI kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) jana katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bruno Selege akitoa elimu ya lishe na mfumo bora wa maisha kwa wananchi wa Mkoa wa Geita waliotembelea katika banda la JKCI kwa ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) jana katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita.


Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophilly Mushi akimuelezea Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) Dkt. Shadrack Mwaibambe namna ambavyo mashine ya ECHO inatumika kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) jana katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita. 


Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Geita wakiwa katika foleni ya kuingia katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu iliyoandaliwa na chama cha Madaktari Tanzania (MAT) jana katika viwanja vya Hospitali ya Mkoa wa Geita. 






















Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari