Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuonyesha Waziri wa Ulinzi wa Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali sehemu ya kusubiria wagonjwa wa kliniki maalumu ya VIP alipotembelea taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa. Waziri wa Ulinzi wa Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali akizungumza na viongozi wa wizara ya Afya, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipozitembelea hospitali hizo leo kwaajili ya kuona namna ambavyo zitawatuma wataalamu wake kwenda kutoa huduma za matibabu ya kibingwa kwa wananchi wa Comoro. Waziri wa Ulinzi wa Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mhandisi Ismail Rumatila mara baada ya kukutana na viongozi wa wizara hiyo, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) na...
Comments
Post a Comment