Posts

Showing posts from August, 2022

Wachangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

Image
Afisa Uuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) Salma Jummanne akimtoa damu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa zoezi lililofanyika leo la uchangiaji damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo. Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi katika zoezi la  kuchangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo. Afisa Uuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) John Juma   akimpima wingi wa damu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)   Dkt. Delila Kimambo wakati zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi  wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakichangia   damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo iliyopo ji...

Kwa mara ya kwanza JKCI yafanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa kufungua tundu dogo kwenye kifua (Minimal Invasive Surgery)

Image
Madaktari bingwa wa upasuaji mkubwa wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya King Faisal Specialist iliyopo nchini Saud Arabia kumfanyia upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu (Bypass Surgery) mgonjwa wakati wa kambi maalum ya siku 6 ya matibabu ya moyo iliyofanyika katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam Madaktari bingwa wa upasuaji mkubwa wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya King Faisal Specialist iliyopo nchini Saud Arabia kumfanyia upasuaji wa kubadilisha mshipa mkubwa wa moyo (aneurysm repair) mgonjwa wakati wa kambi maalum ya siku 6 ya matibabu ya moyo iliyofanyika katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam Daktari bingwa wa usingizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Loth akihakikisha Valvu iliyopandikizwa inafanya kazi vizuri kwa kutumia mashine ya Trans esophageal Echo kabla ya kutoa moyo katika mashine y...

Wataalam wa afya jitokezeni kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi 2022: Mhe. Dkt. Alice Kaijage

Image
Mbunge wa viti Maalum Mhe. Dkt. Alice Kaijage akielezea ujuzi atakaoupata katika mafunzo ya upimaji wa jinsi moyo unavyofanya kazi kwakutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) yatakavyomsaidia katika taaluma yake wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yanayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Jijini Dar Es Salaam. ******************************************************************************************************************************** Wataalam wa afya nchini wameombwa kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kujitokeza na kuwaeleza wagonjwa wanaowahudumia umuhimu wa sense ya watu na makazi kwa maendeleo ya nchi. Akizungumza wakati wa mafunzo ya jinsi ya kufanya kipimo cha kuangalia moyo unavyofanya kazi kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) leo Jijini Dar es Salaam Mbunge wa viti maalum Mhe. Dkt. Alice Kaijage alisema kuwa kwa maendeleo ya taifa lazima kuwe na takwimu hivyo ni vyema watu waka...

Wataalam wa afya nchini wapatiwa mafunzo ya kimataifa ya jinsi ya kufanya kipimo cha kuangalia moyo unavyofanya kazi kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO)

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi kwa kutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) yanayoendelea katika Taasisi hiyo Jijini Dar Es Salaam. Mafunzo hayo yaliyoudhuriwa na wataalam wa afya zaidi ya 100 yamefanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini. Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo na utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akielezea namna mafunzo ya Echo yatakavyofanyika kwa washiriki wa mafunzo ya upimaji wa jinsi moyo unavyofanya kazi kwakutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) yanayoendelea katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam  Mbunge wa viti Maalum Mhe. Dkt. Alice Kaijage akielezea ujuzi atakaoupata katika mafunzo ya upimaji wa jinsi moyo unavyofanya kazi kwakutumia mashine ya Echocardiogram (ECHO) yatakavyomsaidia katika taaluma yake wakati wa mafunzo hayo ya siku mbili yanayoendelea katika Taasisi ya Moyo Ja...

Naibu Waziri wa Afya kutoka nchini Malawi ajifunza utoaji wa huduma za matibabu ya moyo nchini

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.  Mohamed Janabi akielekeza huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa ugeni wa Naibu Waziri wa Afya kutoka nchini Malawi Mhe. Enock Phale kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia mifumo ya Tehama inayotumika katika uendeshaji wa Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akielezea huduma zinazotolewa katika chumba cha upasuaji mkubwa wa moyo kwa Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel pamoja na Naibu Waziri wa Afya Nchini Malawi Mhe. Enock Phale wakati wa ziara yake katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kuangalia mifumo ya Tehama inayotumika katika uendeshaji wa Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya Nchini Malawi Mhe. Enock Phale akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo H...

Wasimamizi wa Mikataba ya Ununuzi JKCI wapatiwa mafunzo

Image
Mwezeshaji kutoka Bodi ya wataalam wa Ugavi na Ununuzi (PSPTB) Jakson Musiba akitoa mafunzo ya jinsi ya kusimamia mikataba ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa wasimamizi wa mikataba ya ununuzi ya Taasisi hiyo leo katika Ukumbi wa JKCI uliopo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ugavi na Ununuzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Idd Lema akiwaelekeza wasimamizi wa mikataba ya ununuzi ya JKCI namna ya kutekeleza majukumu yao wakati wa mafunzo ya jinsi ya kusimamia mikataba ya JKCI yaliyofanyika leo katika Ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam. Wasimamizi wa mikataba ya Ununuzi ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mafunzo yaliyokua yakiendelea ya namna ya kusimamia mikataba ya Taasisi hiyo leo katika Ukumbi wa JKCI uliopo Jijini Dar es Salaam Picha na: Khamis Mussa ************************************************************************************************* Na: Genofeva Matemu Wasimamizi wa mikataba ya Ununuzi ya Taasisi ya Mo...

CRDB Marathon yachangia milioni 250,000,000 matibabu ya moyo kwa watoto

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango akimkabidhi kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo hundi ya shilingi milioni 250 iliyotolewa leo katika Viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB fedha zilizokusanywa kutoka kwa washiriki wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto 125 wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwaongoza viongozi wengine katika matembezi ya kilometa 5 wakati wa mbio za CRDB Marathon kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI na wanawake wenye ujauzito hatarishi wanaotibiwa CCBRT leo Jijini Dar es Salaam Washiriki wa mbio za CRDB Marathon wakishiriki mazoezi ya viungo mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo zilizofanyika katika Viwanja vya Farasi Oyster bay leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchangia watoto 125 wenye magonjwa ya moyo wanao...

Taarifa ya Utekelezaji wa bajeti

Image
 

Prof. Janabi: Wanaume ombeni nafasi za kushiriki mafunzo mbalimbali

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizundua mpango mkakati wa mwaka 2022/23 -2025/2026 wa taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuzindua mpango huo iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa JKCI jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akielezea mpango mkakati wa mwaka 2022/23 -2025/2026 wa JKCI jinsi utakavyofanya kazi kwa viongozi wa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuzindua mpango huo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga wakati akiwaelezea kuhusu mkakati wa taasisi hiyo mwaka 2022/23 -2025/2026. Mwenyekiti wa kamati iliyoandaa mpango mkakati wa mwaka 2022/23 -2025/2026 wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akielezea namna ambavyo mpango mkakati huo umelenga kuboresha huduma zinazotolew...