Wataalam wa afya jitokezeni kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi 2022: Mhe. Dkt. Alice Kaijage
Mbunge wa viti Maalum Mhe. Dkt.
Alice Kaijage akielezea ujuzi atakaoupata katika mafunzo ya upimaji wa jinsi moyo unavyofanya kazi kwakutumia
mashine ya Echocardiogram (ECHO) yatakavyomsaidia katika taaluma yake wakati wa
mafunzo hayo ya siku mbili yanayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
iliyopo Jijini Dar Es Salaam.
********************************************************************************************************************************
Wataalam wa afya nchini wameombwa
kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa
kuwa mstari wa mbele kujitokeza na kuwaeleza wagonjwa wanaowahudumia umuhimu wa
sense ya watu na makazi kwa maendeleo ya nchi.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya
jinsi ya kufanya kipimo cha kuangalia moyo unavyofanya kazi kwa kutumia mashine
ya Echocardiogram (ECHO) leo Jijini Dar es Salaam Mbunge wa viti maalum Mhe.
Dkt. Alice Kaijage alisema kuwa kwa maendeleo ya taifa lazima kuwe na takwimu
hivyo ni vyema watu wakajitokeza kwa pamoja kuhesabiwa
“Kama madaktari inatupasa kujua idadi
ya wagonjwa tunaowahudumia ili tuje kutoa takwimu sahahi ambazo zitaisaidia
serikali kuweka miundombinu rafiki katika maeneo husika kulingana na idadi ya
watu na kuwapa watanzania fursa ya kupata huduma za afya zilizo bora”,
“Sensa ya mwaka huu imedhamiria
kuisaidia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia katika maendeleo ya
nchi pamoja na kuleta mageuzi katika sekta ya afya na jamii hivyo ni wakati
wetu sasa kuhakikisha kuwa takwimu zinazopatikana wakati wa sensa ni sahihi
hivyo kuboresha sekta yetu afya”, alisema
Mhe. Dkt. Alice
Akizungumzia zoezi la Sensa ya watu
na makazi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.
Mohamed Janabi alisema kuwa wataalam wa sekta ya afya ni muhimu kujua idadi ya
watu kwasababu kuna baadhi ya magonjwa ambayo yanakwenda na rika kama
yatapatiwa matibabu katika rika husika hivyo kuwaomba wananchi kuwa mstari wa
mbele kutimiza adhma ya sense ya mwaka 2022 kwa maendeleo endelevu ya afya
nchini
“Zoezi la Sensa litatusaidia sisi
wataalam wa afya kupata takwimu halisi ya watanzania ili kuweka miundombinu ya
afya itakayokidhi huduma za afya kwa watanzania wote”,
“Mfano hai, Tanzania kwa miaka mitano
iliyopita kila mwaka wanazaliwa watoto milioni 2 ambapo kati ya hao asilimia
0.8 mpaka asilimia 1 ya watoto wanazaliwa na tatizo la moyo, na katika hiyo
asilimia 1 asilimia 25 watahitaji upasuaji wa moyo, hivyo nisingekuwa na ile
takwimu ya milioni 2 nisingeweza kupiga hizo hesabu, tutumie tarehe 23 Agosti
kutimiza lengo la kupata takwimu ya watu na makazi nchini”, alismea Prof.
Janabi
Sensa ya watu na makazi ni zoezi la
kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka kumi, ambapo sense ya mwaka 2022 ni sense
ya sita kufanyika nchini baada ya muungano wa Tanganika na Zanzibari mwaka
1964.
Comments
Post a Comment