Wachangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

Afisa Uuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) Salma Jummanne akimtoa damu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati wa zoezi lililofanyika leo la uchangiaji damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi katika zoezi la  kuchangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo.

Afisa Uuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) John Juma  akimpima wingi wa damu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Dkt. Delila Kimambo wakati zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi  wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakichangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi  wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na ndugu wa wagonjwa wakichangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi  wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) pamoja na ndugu wa wagonjwa wakichangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) likiendelea.

Picha na  Khamisi Mussa


Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI kutanua huduma za matibabu ya moyo nchini