JKCI yapongezwa kwa kutoa huduma bora kwa wateja katika maonesho ya SABASABA
Mkurugenzi wa Fedha na
Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Agnes Kuhenga akimkabidhi
zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili
(MOI) Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya alipotembelea banda la JKCI wakati wa
maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA)
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo
barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Dkt. Mpoki
Ulisubisya akimsikiliza Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Emmanuel Lingido alipotembelea banda la JKCI katika maonesho ya 50 ya Biashara
ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Dkt. Mpoki
Ulisubisya akizungumza na daktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Thabit Ramadhani alipotembelea banda la JKCI lililopo
katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA)
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo
barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Agnes Kuhenga na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa JKCI wanaoshiriki katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Na JKCI
***************************************************************************************************
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Mhe. Balozi Dkt. Mpoki
Ulisubisya ameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ubunifu na kuwa
darasa muhimu la elimu ya afya na mfano wa utoaji wa huduma bora kwa wateja katika
Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA).
Dkt. Ulisubisya alisema
kutembelea kwake katika banda la JKCI kumemfungua macho kuona namna huduma
zinazopatikana hospitalini zinavyoweza kutolewa katika maonesho bila kuathiri
utoaji wa huduma kwa wananchi wanaohitaji matibabu katika taasisi hiyo kwani
JKCI imejipanga vizuri kupokea wananchi na kutoa huduma mbalimbali ikiwemo
vipimo kwa ubora unaolingana na huduma zinazotolewa katika matawi yake.
Aidha Dkt. Ulisubisya
alisema uchangamfu na weledi wa wataalamu wa JKCI umemvutia akieleza kuwa kwa
sasa taasisi nyingi zinahitaji kuimarisha huduma bora kwa wateja kama ambavyo
JKCI inafanya kwani kila anayefika katika banda hilo hupokelewa vizuri, kupewa
maelezo ya kutosha na kuondoka akiwa amepata elimu ya kina kuhusu magonjwa ya
moyo pamoja na umuhimu wa lishe bora.
“Uwepo wa banda la JKCI
katika maonesho haya ni hatua muhimu ya kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni
wa kuchunguza afya zao mara kwa mara badala ya kusubiri hadi wanapougua ndipo
waende hospitalini kwani elimu inayotolewa katika banda hili inaweza kusaidia
kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu kinga na utambuzi wa mapema wa magonjwa ya
moyo”, alisema Dkt. Ulisubisya.



.jpeg)

Comments
Post a Comment