Prof. Kabudi; Watanzania jivunieni kuwa na JKCI, Ni Taasisi ya umahiri Barani Afrika

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Profesa Palamagamba Kabudi akipimwa joto la mwili na Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jackline Mwaipopo alipotembelea katika banda la JKCI wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Profesa Palamagamba Kabudi akimsikiliza Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Emmanuel Lingido alipotembelea banda la JKCI wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Profesa Palamagamba Kabudi akipokea zawadi kutoka kwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mohamed Aloyce alipotembelea banda la JKCI wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edna Kajuna akimuonesho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Profesa Palamagamba Kabudi betri ya moyo (Pace maker) alipotembelea banda la JKCI wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Profesa Palamagamba Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na  wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wanaoshiriki katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Na JKCI

***********************************************************************************************

Watanzania wametakiwa kujivunia uwepo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwani ni taasisi ya umahiri katika Bara la Afrika inayotoa huduma za kisasa za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa viwango vya kimataifa.

Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Prof. Palamagamba Kabudi alipotembelea banda la JKCI katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (SABASABA) ambapo aliwataka watanzania kuitumia taasisi hiyo na kuiunga mkono hususan katika kampeni yake ya kuwasaidia watoto wenye magonjwa ya moyo ili waweze kupata matibabu na kuendelea kutimiza ndoto zao.

Prof. Kabudi aliipongeza JKCI kwa huduma zake za kisasa za tiba ya moyo, akisema ameridhishwa na kiwango cha utaalamu alichokiona pamoja na uwepo wa wataalamu wabobezi wanaotoa huduma na elimu kwa wananchi katika maonesho hayo hatua ambayo inaonesha dhamira ya taasisi hiyo ya kuwafikia watanzania popote walipo na kuwapatia huduma za kibingwa.

Aidha Prof. Kabudi alizitaka hospitali nyingine nchini kuiga kampeni ya “Jua Namba Zako” ambayo inalenga kuwahamasisha wananchi kufahamu viashiria muhimu vya afya zao ili kusaidia kinga na utambuzi wa mapema wa magonjwa ya moyo na magonjwa mengine yasiyoambukiza.

Prof. Kabudi alisisitiza kuwa huduma zinazotolewa na JKCI ni za kiwango cha juu na zinawafikia watanzania wa makundi yote bila ubaguzi hivyo kuimarisha afya ya jamii na kuongeza uelewa kuhusu kinga na matibabu ya magonjwa ya moyo.

 

Comments

Popular posts from this blog

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi