Kambi ya matibabu ya moyo yaokoa milioni 493

Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Africa la nchini Marekani kumfanyia upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo wa Cath lab mgonjwa mwenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu hayo leo jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 15 wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wamepatiwa matibabu katika kambi hiyo. Wataalamu wa afya ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Cardiography - ECHO) mgonjwa ambaye ana matatizo za mfumo wa umeme wa moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu hayo leo jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 15 wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wamepatiwa matibabu katika kambi hiyo. Wataalamu wa afya ya Taasisi Ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakiandaa vifaa kwa ajili ya kumfanyia upasuaji wa moyo ...