JKCI yasaini mkataba wa kutibu wagonjwa wa moyo wa Zambia na Rwanda
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia Dkt. Shumba Chabwela wakisaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu wa kutibu wagonjwa wa moyo wa nchini Zambia na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya wa hospitali hiyo wa jinsi ya kuwatibu wagonjwa wa moyo. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakipongezana na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia Dkt. Shumba Chabwela mara baada ya kusaini mkataba wa kutibu wagonjwa wa moyo na kuwajengea uwezo wa kuwatibu wagonjwa wa moyo wataalamu wa afya wa hospitali hiyo. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Naibu Mtendaji Mkuu Hospitali ya King Faisal ya nchini Rwanda Frederic Ngirabacu wakisaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu wa kutibu wagonjwa wa moyo na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya wa hospitali hiyo wa jinsi ya kuwatibu wagonjwa wa moyo. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Naibu Mtendaji Mkuu Hospitali ya King Faisal ya nchini Rwanda Frederic Ngirabacu wakionesha mkataba wa kutibu wagonjwa wa moyo na kuwajengea uwezo wa kuwatibu wagonjwa wa moyo wataalamu wa afya wa Hospitali hiyo. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza namna ambavyo Tanzania imepiga hatua katika kutoa huduma za matibabu ya moyo wakati Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ilipokuwa ikisaini mkataba wa kutibu wagonjwa wa moyo pamoja na kuwafundisha wataalamu wa afya wa Hospitali za Taifa za moyo za nchini Rwanda na Zambia leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu akizungumza wakati Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikisaini mkataba wa kutibu wagonjwa wa moyo na kuwajengea uwezo wa jinsi ya kuwatibu wagonjwa wa moyo wataalamu wa Hospitali za Taifa za moyo za nchini Rwanda na Zambia leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akielezea namna ambavyo taasisi hiyo inapokea wagonjwa kutoka nchi mbalimbali za Afrika kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali wakati JKCI ilipokuwa ikisaini mkataba wa kutibu wagonjwa wa moyo na kuwajengea uwezo wa jinsi ya kuwatibu wagonjwa wa moyo wataalamu wa afya wa Hospitali za Taifa za moyo za nchini Rwanda na Zambia leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya King Faisal ya nchini Rwanda, Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel mara baada ya JKCI kusaini mkataba na nchi za Zambia na Rwanda wa kuwatibu wagonjwa wa moyo pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya wa hospitali hizo.
***********************************************************************************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imesaini mikataba ya miaka mitatu ya makubaliano na Hospitali za Taifa za nchini Rwanda na Zambia kutibu wagonjwa wa moyo pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa afya wa hospitali hizo wa jinsi ya kuwatibu wagonjwa wa moyo.
Naye mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. William Mahalu alisema utendaji kazi wa JKCI unaonekana hivyo ni imani yake kuwa kwa kusaini mkataba na nchi hizo mbili kutatoa motisha kwa nchi nyingine za Afrika kuona umuhimu wa kushirikiana na KCI.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child's Heart - SACH) la nchini Israel Simon Fisher alisema kupitia Taasisi hiyo wameweza kuwaunganisha Rwanda na Zambia kushirikiana na JKCI kuwasaidia watoto wanaohitaji huduma za matibabu ya moyo.
Fisher alisema anajivunia kushuhudia huduma za kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo inafanyika JKCI, ikifanywa na Dkt. Godwin Sharau ambaye ni daktari wa kwanza wa upasuaji wa moyo wa watoto aliyepata mafunzo nchini Israel.
"Kwa kuwa sasa JKCI imekuwa kituo cha ubora kusini mwa jangwa la Sahara, shughuli zetu za kujenga uwezo zimeongezeka maradufu na sasa tumeongeza vituo viwili yaani Rwanda na Zambia", alisema Fisher.
Comments
Post a Comment