Wataalam wa JKCI wawafundisha wataalam wa Chato jinsi ya kutumia mashine ya Ventilator
Daktari Bingwa wa Usingizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Faraji Lydenge na Afisa Uuguzi wa JKCI Ally Athuman wakiwafundisha
wataalam wa afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda chato (CZRH) na Hospitali
ya Wilaya ya Chato namna ya kutumia mashine ya kumsaidia mgonjwa kupumua
(Ventilator) wakati wa mafunzo ya siku tatu yaliyotolewa na wataalam wa JKCI
katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato.
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) Dkt. Brian Mawala akizungumza na
washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya kutumia mashine ya kumsaidia mgonjwa
kupumua (Ventilator) yaliyofanywa na wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) na kumalizika hivi karibuni.
Daktari
bingwa wa wagonjwa mahututi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Vivian
Mlawi akiwafundi wataalam wa afya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda chato
(CZRH) na Hospitali ya Wilaya ya Chato namna ya kutumia mashine ya kumsaidia
mgonjwa kupumua (Ventilator) kabla ya kuanza mafunzo kwa vitendo wakati wa
mafunzo ya siku tatu yaliyotolewa na wataalam wa JKCI katika Hospitali ya Rufaa
ya Kanda Chato.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) Dkt.
Brian Mawala akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tatu
ya kutumia mashine ya kumsaidia mgonjwa kupumua (Ventilator) yaliyofanywa na
wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kumalizika
hivi karibuni.
**************************************************************************************************************************
Comments
Post a Comment