Iringa kufaidika na huduma za matibabu ya moyo
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akizungumza na wakazi wa Iringa kuhusu mfumo bora wa maisha wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari bingwa wa moyo kutoka JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH). Kambi hiyo ya siku tano itamalizika siku ya ijumaa 7 Aprili 2023
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimsomea majibu mkazi wa Iringa Sulle Ayubu mara baada ya kufanya vipimo vya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magreth Ng’ondya akimwelezea mkazi wa Iringa Lucas Ngailo umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalam kutoka JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH)
Na: JKCI
*************************************************************************************************************
Comments
Post a Comment