Wagonjwa 10 kutibiwa mfumo wa umeme wa moyo



Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Africa  la nchini Marekani kumfanyia  upasuaji wa tundu dogo kwa kutumia mtambo  wa Cath lab mgonjwa mwenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu hayo leo jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 10 wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi hiyo.


Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakiangalia umeme wa moyo unaoingia kwa mgonjwa unavyofanya kazi kwa kutumia mashine ya CRTD Programmer  wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu hayo leo jijini Dar es Salaam. Wagonjwa 3 kati ya 10 wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wameshafanyiwa upasuaji katika kambi hiyo.

********************************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa