Kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya moyo yafanyika Iringa
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Elizabeth
Meli akimpima shinikizo la damu mwilini (BP) raia wa Switzerland Lans Sottwals aliyefika
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH) leo kwa ajili ya kupata
huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano
inayofanywa na wataalam hao kwa kushirikiana na wenzao wa IRRH.
Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Loveness
Mfanga akimfanyia utafiti mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Iringa (IRRH) kwa ajili ya kupata huduma ya uchunguzi na matibabu ya moyo
leo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Hospitali
hiyo. Kambi hiyo ya siku tano inafanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana
na wenzao wa IRRH
Na: JKCI
*********************************************************************************************************
Wananchi
wa Mkoa wa Iringa wametakiwa kutumie fursa ya uwepo wa madaktari bingwa wa moyo
kujitokeza kwa wingi kuchunguza moyo kupitia kambi maalum inayofanywa na
madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Rai
hiyo imetolewa leo na Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH)
Dkt. Alfred Mwakalebela wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo inayofanyika kwa siku
tano lengo likiwa ni kufikisha huduma karibu kwa wananchi.
Dkt.
Mwakalebela alisema kupitia kambi hiyo wananchi watapata fursa ya kupimwa
vipimo vyote vikubwa vya moyo, kupata dawa kwa wale watakaokutwa na magonjwa ya
moyo na wengine watakaohitaji uchunguzi zaidi watapewa rufaa kwa ajili ya
uchunguzi zaidi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
“Tukipata
wataalamu kama hawa katika Hospitali yetu kunasaidia kuwachunguza kwa kina
zaidi wagonjwa na baada ya hapo wataalam hawa watatuachia wagonjwa hao kwa
ajili ya kuendelea na kliniki hapa kwetu hivyo kupunguza tatizo kwa kiasi kikubwa
tofauti na ilivyokuwa awali”, alisema Mwakalebela
Dkt.
Mwakalebela alisema kupitia wataalam waliotoka JKCI wanaenda kuwaonyesha njia
wataalam wa IRRH ya namna ya kuwachunguza wagonjwa wa moyo pamoja na
kuwafuatilia mara kwa mara ili kwapamoja waweze kuwafuatilia kwa karibu na
kuwapa huduma stahiki.
“JKCI
imekuwa na utaratibu wa kupeleka huduma karibu na wananchi ili waweze kupata
huduma kwa urahisi zaidi na sasa ni zamu yetu wananchi wa Mkoa wa Iringa,
tunaahidi kushirikiana nao kuwasaidia wananchi wetu”, alisema Mwakalebela
Kwa
upande wake Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallagyo
alisema magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndio yanayoongoza kwa kusababisha vifo vingi
ulimwenguni na katika mazingira ya Tanzania magonjwa hayo yanaonekana
yakiongezeka kwa kasi.
“Wataalam
wa JKCI tupo Iringa kwa ajili ya kufanya vipimo na huduma za kibingwa za moyo
hivyo tukiwa na utaratibu wa kuchunguza afya zetu na kugundua mapema inakuwa
rahisi kutibu na kuwa na matokeo mazuri zaidi”, alisema Dkt. Pedro
Dkt.
Pedro alisema mwamko wa wananchi kuchunguza afya zao bado uko chini lakini
kupita kambi maalum za matibabu ya moyo wanazofanya toka wameanza mwitikio
umekuwa ukiongezeka huku lengo likiwa kuwasaidia wagonjwa na kujenga desturi
kwa watu kuwa wanachunguza afya zao mara kwa mara.
Naye
mwananchi aliyepatiwa huduma katika kambi hiyo Gerald Isambo alisema amekuwa
akisumbuliwa na tatizo la kifua mara kwa mara na kutokupata utatuzi nini
kinachomsumbua hivyo kupitia kambi hiyo amepata fursa ya kupima moyo wake.
Isambo
alisema kuwa hakuwahi kupima moyo tangu kuzaliwa kwake hivyo fursa hiyo
aliyoipata imempa mwamko wa kufanya uchunguzi wa afya yake mara kwa mara na
kuacha tabia ya kuchuguza afya yake pale tu anapoumwa.
“Naomba
kupitia Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa huduma kama hizi na nyingine
za kibingwa ziendelee kutolewa mara kwa mara kutupa nafasi sisi wananchi ambao
hatuwezi kuzifuata mahali zilipo kuchunguza afya zetu na kuwa na desturi ya kujichunguza”,
alisema Isambo
Comments
Post a Comment