Posts

Showing posts from January, 2024

China kuleta vifaa tiba nchini

Image
Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Watu wa China Mhe. Liu Guozhong alipofanya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kuona huduma zinazotolewa.  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuelezea mafanikio ya Taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Watu wa China Mhe. Liu Guozhong alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo kuona huduma zinazotolewa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuelezea huduma zinazotolewa katika chumba cha upasuaji wa tundu dogo (CathLab) Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Watu wa China Mhe. Liu Guozhong alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo kuona huduma zinazotolewa. Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Watu wa China Mhe. Liu Guozhong na viongozi wengine wa Serikali mara baada ya ziara ya Naibu Waziri Mk

JKCI yafanya upasuaji wa moyo kwa watoto saba wa Zambia

Image
Madaktari wa Usingizi na Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakimlaza mtoto kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi ya matibabu iliyomalizika jana nchini Zambia. Kambi hiyo ya siku tatu na nusu imewezeshwa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel. Wataalamu wa afya wanaofanya kazi katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakijaza fomu ya maendeleo ya mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi ya matibabu iliyomalizika jana nchini Zambia. Kambi hiyo ya siku tatu na nusu imewezeshwa na  Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel. *********************************************************************************************************************************************************

Watu 573 wafikiwa na huduma ya tiba mkoba Tabora

Image
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani akizungumza na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati akipokea taarifa ya upimaji wa magonjwa ya moyo ujulikanao kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoa uliokuwa ukifanyika mkoani Tabora na kumalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani akimkabidhi zawadi za wataalamu wa afya waliofanya kambi ya upimaji wa magonjwa ya moyo mkoani humo Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina Kazahura baada ya kumalizika kwa kambi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita. Wapili kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Tabora – KITETE Dkt. Mark Waziri Na: JKCI ********************************************************************************************************* Watu 573 wamepatiwa huduma ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo katika kambi maalumu ya matibabu ijulikanayo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services iliyofanywa

Tanzania kuendelea kushirikiana na Zambia katika upasuaji wa moyo

Image
  Afisa muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) anayefanya kazi katika chumba cha upasuaji wa moyo Fredy Tupa akiwaelekeza wenzake wa hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia namna ya kuandaa vifaa vyakufanyia upasuaji wakati wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo inayofanyika nchini Zambia. Kambi hiyo ya upasuaji imewezeshwa na  Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) anayefanya kazi katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) Kelvin Mutta na Afisa muuguzi wa Taasisi hiyo Mohamed Wamara wakimuhudumia mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalumu ya matibabu inayofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia. Kambi hiyo ya upasuaji imewezeshwa na  Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) anayefanya kazi katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) Kelv

Waiomba Serikali matibabu ya moyo kufanyika mara kwa mara

Image
  Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina Kazaula akimpima jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph – ECHO) mtoto mwenye tundu kwenye moyo wakati wa kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE. Afisa Uuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE Backford John akimpima wingi wa sukari mwilini mwananchi wa mkoa wa Tabora aliyefika katika Hospitali hiyo kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Na: JKCI ************************************************************************************************************ Wananchi wa Mkoa wa Tabora wameiomba serikali kufikisha huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo mara kwa mara katika mkoa huo

Watoto 10 kufanyiwa upasuaji wa moyo Zambia

Image
Wataalamu wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakimfanyia mtoto upasuaji wa kuziba tundu la moyo katika kambi maalumu ya upasuaji inayofanyika nchini Zambia. Watoto 10 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wanatarajia kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku tatu ambayo imewezeshwa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel.   Wataalamu wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakipongezana mara baada ya kumaliza kumfanyia mtoto upasuaji wa kuziba tundu la moyo katika kambi maalumu ya upasuaji inayofanyika nchini Zambia. Watoto 10 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wanatarajia kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ambayo imewezeshwa na  Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel. Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

Image
Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew Edward Mkingule akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya wataalamu hao kuanza safari  ya  kuelekea katika hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia kwaajili ya kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto. Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel ndilo lililowezesha kufanyika kwa kambi hiyo ya upasuaji nchini Zambia. Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni  Generali Mathew  Edward  Mkingule akizungumza na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Julius Nyerere  (JNIA)  kabla ya kuanza safari yao ya kwenda katika hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia kwaajili ya kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto.  Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel ndilo lililowezesha kufanyika kwa kambi hiyo ya upa

Wananchi wa Tabora wajitokeza kupima moyo

Image
Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sigfrid Shayo akimpima mgonjwa shinikizo la damu (BP) wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Samia Suluhu Hassan outreach services inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE. Afisa lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akiwafundisha wananchi wa mkoa wa Tabora umuhimu wa kutumia makundi yote ya vyakula wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Samia Suluhu Hassan outreach services inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE. Afisa Uuguzi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE Izadini Mohamed akimpima shinikizo la damu mwananchi wa mkoa wa Tabora aliyefika katika Hospitali hiyo kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano inayofanywa na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali

Dkt. Batilda Buriani: Changamkieni fursa ya kupima moyo

Image
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani akizungumza na madaktari bingwa wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) waliofika katika Mkoa wa Tabora kwaajili ya kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa mkoa huo. Kambi hiyo maalumu ijulikanayo kama Mhe. Samia Suluhu Hassan Outreach services ya siku tano imeanza leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE Dkt. Mark Waziri akitoa neno la shukrani kwa madaktari bingwa wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuwafikia wananchi wa Tabora wakati wa kuwapokea madaktari hao leo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora kabla ya kuanza kambi maalumu ya matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Samia Suluhu Hassan Outreach services ya siku tano inayofanywa na madaktari hao. Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mratibu wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Samia Suluhu Hassan

Madaktari bingwa kutoka China waendelea kutoa huduma za matibabu nchini

Image
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo akizungumza na madaktari kutoka Serikali ya Watu wa China alipokuwa akimuwakilisha Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel kwenye hafla fupi ya kuwaaga madaktari kutoka China kundi la 26 na kuwakaribisha madaktari kundi la 27 jana katika Chuo cha Utalii kilichopo jijini Dar es Salaam. Serikali ya Watu wa China imekuwa ikileta madaktari nchini kila baada ya miaka miwili ili kubadalishana ujuzi na madaktari wa Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akitoa neno la shukrani kwa madaktari kutoka Serikali ya Watu wa China kundi namba 26 waliokuwa wanafanya kazi JKCI na kuwakaribisha madaktari kundi namba 27 wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana katika Chuo cha Utalii kilichopo jijini Dar es Salaam.   Mkuu wa masuala ya ushirikiano kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Suo Peng akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari kutoka China kundi la 26 na kuwakari