Wananchi wa Tabora wajitokeza kupima moyo

Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sigfrid Shayo akimpima mgonjwa shinikizo la damu (BP) wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Samia Suluhu Hassan outreach services inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE.


Afisa lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akiwafundisha wananchi wa mkoa wa Tabora umuhimu wa kutumia makundi yote ya vyakula wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Samia Suluhu Hassan outreach services inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE.

Afisa Uuguzi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE Izadini Mohamed akimpima shinikizo la damu mwananchi wa mkoa wa Tabora aliyefika katika Hospitali hiyo kwaajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano inayofanywa na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya KITETE. 


Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Tabora wakisubiri kupata huduma wakati wa kambi maalumu ya siku tano inayofanywa na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya KITETE.

Picha na: JKCI

*************************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024