Madaktari bingwa kutoka China waendelea kutoa huduma za matibabu nchini


Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo akizungumza na madaktari kutoka Serikali ya Watu wa China alipokuwa akimuwakilisha Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel kwenye hafla fupi ya kuwaaga madaktari kutoka China kundi la 26 na kuwakaribisha madaktari kundi la 27 jana katika Chuo cha Utalii kilichopo jijini Dar es Salaam. Serikali ya Watu wa China imekuwa ikileta madaktari nchini kila baada ya miaka miwili ili kubadalishana ujuzi na madaktari wa Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akitoa neno la shukrani kwa madaktari kutoka Serikali ya Watu wa China kundi namba 26 waliokuwa wanafanya kazi JKCI na kuwakaribisha madaktari kundi namba 27 wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana katika Chuo cha Utalii kilichopo jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa masuala ya ushirikiano kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Suo Peng akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari kutoka China kundi la 26 na kuwakaribisha madaktari kundi la 27 jana katika Chuo cha Utalii kilichopo jijini Dar es Salaam. Serikali ya Watu wa China imekuwa ikileta madaktari nchini kila baada ya miaka miwili kubadalishana ujuzi na madaktari wa Tanzania.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akimpatia zawadi Daktari kutoka Serikali ya Watu wa China aliyefanya kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miaka miwili Sun Xufang wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari kutoka China kundi la 26 na kuwakaribisha madaktari kundi la 27 jana katika Chuo cha Utalii kilichopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akimkaribisha Daktari kutoka Serikali ya Watu wa China anayekwenda kufanya kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zhang Mingming wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari kutoka China kundi la 26 na kuwakaribisha madaktari kundi la 27 jana katika Chuo cha Utalii kilichopo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya madaktari kutoka Serikali ya Watu wa China kundi la 27 waliofika nchini kwaajili ya kubadilishana ujuzi na madaktari wa Tanzania wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari kutoka China kundi la 26 na kuwakaribisha madaktari kundi la 27 jana katika Chuo cha Utalii kilichopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na madaktari kutoka Serikali ya Watu wa China wanaofanya kazi na JKCI wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari kutoka China kundi la 26 na kuwakaribisha madaktari kundi la 27 jana katika Chuo cha Utalii kilichopo jijini Dar es Salaam.

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari