Posts

Showing posts from August, 2024

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina tuzo ya taasisi ambayo imetoa  mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 tuzo hiyo ameitoa wakati  akifungua kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za umma kinachofanyika jijini Arusha. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Angela Muhozya. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Angela Muhozya kabla ya kuwakabidhi  tuzo ya taasisi ambayo imetoa  mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024. Tuzo hiyo imetolewa leo jiji Arusha wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa Taas

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

Image
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Arusha kuhusu wataalamu wa Taasisi hiyo na wenzao wa hospitali ya AICC Arusha kutoa huduma za ushauri, upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wenyeviti na watendaji wakuu wa taasisi za umma watakaoshiriki kikao kazi kitakachofanyika jijini humo. Kikao kazi hicho cha siku tatu kimeandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina. Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Arusha kuhusu wataalamu wa Taasisi hiyo na wenzao wa hospitali ya AICC Arusha kutoa huduma za ushauri, upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wenyeviti na watendaji wakuu wa taasisi za umma watakaoshiriki kikao kazi kitakachofanyika jijini humo. Kikao kazi hicho cha siku tatu kimeandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina. Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya AICC Arusha Dkt. Ezekiel Moirana akizungumza na w

JKCI yatoa mafunzo kwa wauguzi kutoka nchini Zambia

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wauguzi kutoka nchini Zambia waliohitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpongeza Afisa Muuguzi kutoka nchini Zambia Christine Musonda aliyehitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKDI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na maafisa Uuguzi kutoa nchini Zambia waliohitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo wakati wa kuwaaga jijini

JKCI kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo nchini Congo

Image
******************************************************************************************************************* Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeombwa kufanya kambi maalumu ya matibabu ya moyo nchini Congo pamoja na kuendelea kukuza umoja na ushirikiano katika sekta ya afya na utalii matibabu.    Rai hiyo imetolewa jana na Balozi wa Congo nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Massala alipotembelea Taasisi hiyo leo na kuona fursa zinazopatikana ikiwemo ushirikiana uliojengwa nan chi mbalimbali duniani. Mhe. Balozi Massala alisema kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Congo na Tanzania katika nyanja mbalimbali ni vyema sasa ushirikiano mkubwa ukawekezwa katika sekta ya afya na kutoa fursa kwa wataalamu wa afya kutoka Congo na Tanzania kubadilishana ujuzi. “Nimeona mabadiliko makubwa sana ukilinganisha na miaka ya nyuma nilipotembelea hapa, hii ni chachu kwetu sisi kama Congo kushirikiana na ndugu zetu wa Tanzania ili tuweze kujifunza namna wanavyofanya kazi, tunaweza kuwale

Wanafunzi 965 wapimwa moyo Dar es Salaam

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Hospitali ya Shandong Provincial iliyopo nchini China ambaye pia anafanya kazi Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Zhao Lijian akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Msasani wakati wa kambi maalumu ya siku mbili iliyomalizika leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanafunzi 965 wa Shule za Msingi Hananasif na Msasani wamefanyiwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi.  Daktari bingwa wa watoto wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Theophylly Ludovick akizungumza na mzazi ambaye mtoto wake amefanyiwa kipimo cha moyo wakati wa uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa wanafunzi wa Shule ya Misingi Msasani leo jijini Dar es salaam. Jumla ya wanafunzi 965 wa Shule za Msingi Hananasif na Msasani wamefanyiwa kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi.  Daktari kutoka Hospitali ya YUNNAN FUWAI iliyopo nchini China Zhang Shuyue akisikiliza mapigo ya moyo ya mwanafunzi wa Shule ya Msin

JKCI na Hosptiali ya YUNNAN FUWAI ya China zawapima moyo wanafunzi wa shule ya msingi Hananasif

Image
Wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya YUNNAN FUWAI iliyopo nchini China wakawa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Hananasif wakati wa zoezi la upimaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophil Ludovic pamoja na madaktari wenzake kutoka Hospitali ya YUNNAN FUWAI iliyopo nchini China wakipitia majibu ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi baada ya kumfanyia kipimo hicho mwanafunzi wa Shule ya Msingi Hananasif leo jijini Dar es Salaam. Daktari kutoka Hospitali ya YUNNAN FUWAI iliyopo nchini China Zhang Jun akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Hananasif leo jijini Dar es Salaam. JKCI kwa kushirikiana na madaktari kutoka nchini China wanafanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa siku mbili kwa wanafunzi wa shule za msingi Hananasif na Msasani z

Wafanyakazi waliohama JKCI waagwa

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuaga aliyekuwa Mhasibu wa Taasisi hiyo Mohamed Songoro wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi wa JKCI waliopata uhamisho kwenda katika taasisi mbalimbali za umma leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuaga aliyekuwa Katibu Muhtasi wa Taasisi hiyo Faith Temba wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi wa JKCI waliopata uhamisho kwenda katika taasisi mbalimbali za umma leo jijini Dar es Salaam. Aliyekuwa Mfamasia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nelson Faustine akitoa neno la shukrani mara baada ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi wa JKCI waliopata uhamisho kwenda katika taasisi mbalimbali za umma leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo waliopata uham

Mhe. Mhagama: Hakikisheni huduma za matibabu ya kibingwa zinawafikia wananchi wa hali ya chini

Image
  Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ndogo za wizara   hiyo zilizopo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa kuwa waziri wa wizara ya Afya. Naibu Waziri wa Afya  Mhe. Godwin Mollel akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo wakati wanasubiri kumpokea Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama aliyeapishwa  Ikulu jijini Dar es Salaam kuwa waziri wa wizara ya Afya. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya  Bw. Ismail Rumatila akiwasalimia wafanyakazi wa wizara hiyo katika ofisi ndogo za wizara  zilizopo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)  Dkt. Irene Isaka akiwasalimia wafanyazi wa wizara ya Afya wakati wa mkutano na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Jenista Muhagama uliofanyika  katika ofisi ndogo za wizara   zilizopo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama akimsalimia Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Ki

Mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo kufanyika Zanzibar

Image

JKCI yaandaa mkutano wa kimataifa wa moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wadau leo wakati wa uzinduzi wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa magonjwa ya moyo (Cardiotan Africa) utakaofanyika mwezi Aprili 2025 katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo mjini Zanzibar. Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa tatu wa kimataifa wa magonjwa ya moyo (Cardiotan Africa) utakaofanyika mwezi Aprili 2025 katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo mjini Zanzibar Dkt. Delilah Kimambo akielezea malengo ya mkutano huo leo wakati wa uzinduzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi na wadau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia wakati wa uzinduzi wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa magonjwa ya moyo (Cardiotan Africa) uliokuwa ukifanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Taasisi hiyo mara baada ya uzinduzi wa mk

Watu 558 wafanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Mlagwa Yango akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi aliyepatiwa huduma katika kambi maalumu ya siku nne ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika Zahanati ya Bungoni kata ya Ilala na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo imefanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Yona Jeremia akimshauri mwananchi wa Ilala baada ya kufanya vipimo vya magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku nne ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba iliyokuwa ikifanyika katika Zahanati ya Bungoni kata ya Ilala na kumalizika jana jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo imefanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Z