JKCI na Hosptiali ya YUNNAN FUWAI ya China zawapima moyo wanafunzi wa shule ya msingi Hananasif


Wataalamu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya YUNNAN FUWAI iliyopo nchini China wakawa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Hananasif wakati wa zoezi la upimaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophil Ludovic pamoja na madaktari wenzake kutoka Hospitali ya YUNNAN FUWAI iliyopo nchini China wakipitia majibu ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi baada ya kumfanyia kipimo hicho mwanafunzi wa Shule ya Msingi Hananasif leo jijini Dar es Salaam.

Daktari kutoka Hospitali ya YUNNAN FUWAI iliyopo nchini China Zhang Jun akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Hananasif leo jijini Dar es Salaam. JKCI kwa kushirikiana na madaktari kutoka nchini China wanafanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa siku mbili kwa wanafunzi wa shule za msingi Hananasif na Msasani zilizopo jijini Dar es Salaam.


Daktari kutoka Hospitali ya YUNNAN FUWAI iliyopo nchini China Zhao Xing akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Hananasif leo jijini Dar es Salaam. JKCI kwa kushirikiana na madaktari kutoka nchini China wanafanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa siku mbili kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Hananasif na Msasani za jijini Dar es Salaam.


Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophil Ludovic akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Hananasif magonjwa ya moyo kwa watoto wakati wataalamu wa JKCI na wenzao kutoka Hospitali ya YUNNAN FUWAI ya nchini China walipokuwa wakifanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanafunzi wa shule hiyo leo jijini Dar es Salaam.


Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabela Mkojera akimwelekeza jinsi ya kujibu maswali ya ufahamu wa magonjwa ya moyo mwanafunzi wa shule ya msingi Hananasif wakati wataalamu wa JKCI na wenzao wa Hospitali ya YUNNAN FUWAI ya nchini China walipofika shuleni hapo leo kwa ajili ya kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanafunzi wa shule hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Picha na: JKCI
***********************************************************************************************************************
 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari