JKCI yatoa mafunzo kwa wauguzi kutoka nchini Zambia
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimpongeza Afisa Muuguzi kutoka nchini Zambia Christine
Musonda aliyehitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na
mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKDI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na maafisa Uuguzi kutoa nchini Zambia
waliohitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na
mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) leo wakati wa kuwaaga jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi kutoka nchini Zambia Erica Khunga akitoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Maafisa Uuguzi wanne kutoka nchini humo waliokuwa wanachukua mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimpongeza Afisa Uuguzi kutoka nchini Zambia Aoraida Nkhoma
aliyehitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na
mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpongeza Afisa Uuguzi kutoka nchini Zambia Able Kaunda aliyehitimu mafunzo ya miezi sita ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi yanayotolewa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo jijini Dar es Salaam.
Picha na: Hamis Mussa
*********************************************************************************************************************
Na: Stella Gama
Wauguzi kutoka nchini Zambia walioudhuria mafunzo ya
kuwahudumia wagonjwa mahututi na wa dharura wametakiwa kuwa mabalozi wazuri
wanaporejena nchini mwao na kutumia vizuri ujuzi walioupata wanapowahudumia wagonjwa
hao.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa hafla fupi ya kuwaaga
wauguzi hao iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar
es Salaam.
Dkt. Kisenge alisema kupitia mafunzo waliyopata kwa kipindi
cha miezi sita wauguzi hao waono uwezo wa kuokoa maisha ya wagonjwa mahututi
kwani wagonjwa hao wanahitaji uangalizi wa karibu zaidi.
“Kuna nchi nyingi wanatoa mafunzo kama haya, lakini nyie
mmechagua kuyapata hapa kwetu Tanzania hii nikutokana na uhusiano mzuri
tulionao baina ya nchi zetu hizi mbili”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema mbali na kushiriki katika mafunzo hayo
wauguzi hao pia wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio
vilivyopo nchini ikiwa ni sehemu ya kufanya utalii na kujifunza kutoka kwetu.
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo kutoka Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joshua Ogutu alisema kupitia mafunzo waliyopata
wauguzi hao wataenda kubadilisha utoaji wa huduma na kuokoa maisha ya wagonjwa
wanaowahudumia.
Ogutu ambaye pia ni Muuguzi wa JKCI alisema wauguzi hao
wamepitia hatua zote za kuwahudumia wagonjwa wa dharura na mahututi pamoja na
kutumia mashine zinazotumiwa na wagonjwa hao kama vile mashine ya kusaidia
kupumua.
“Kupitia elimu waliyoipata hapa wagonjwa wa dharura
watakaopitia katika mikono yao watakuwa salama kwani hatua zote za kuwahudumia
wagonjwa mahututi zimefanyika kwa vitendo wakati wa mafunzo”, alisema Ogutu
Naye muuguzi kutoka nchini Zambia Erica Khunga aliishukuru
JKCI kwakuanzisha mafunzo hayo kwani yamekuwa na umuhimu kwao kama wauguzi
katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Erica alisema wataendelea kutumia fursa ya mafunzo iliyopo
JKCI kuendelea kujifunza katika maeneo mengine yakutoa huduma kwa wagonjwa
ikiwemo katika chumba cha upasuaji mdogo wa moyo.
“Kupitia mafunzo haya imekuwa mara yangu ya kwanza kutoa
huduma katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu, nilivyokuja ni
tofauti na ninavyoondoka”, alisema Erica.
Mafunzo kwa wauguzi ya kuwahudumia wagonjwa ya dharura na
mahututi yaliyoanza mwezi Machi na kumalizika mwezi Agosti 2024 yanakuwa
mafunzo yakwanza kumalizika JKCI ikiwa inashirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM).
Comments
Post a Comment