Watoto 29 wafanyiwa upasuaji wa moyo JKCI

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dar Group Dkt. Tulizo Shemu na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Yahya Ahmad wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Center cha nchini Saud Arabia wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha kambi maalumu ya upasuajia wa moyo kwa watoto iliyomalizika jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya watoto 29 wamefanyiwa upasuaji wa moyo

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmad wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa JKCI wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha kambi maalumu ya upasuajia wa moyo kwa watoto iliyomalizika jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya watoto 29 wamefanyiwa upasuaji wa moyo 

Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmad akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha kambi maalumu ya upasuajia wa moyo kwa watoto iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Center cha nchini Saud Arabia na kumalizika jana jijini Dar es Salaam.  Jumla ya watoto 29 wamefanyiwa upasuaji wa moyo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha kambi maalumu ya upasuajia wa moyo kwa watoto iliyokuwa ikifanywa na wataalamu JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Center cha nchini Saud Arabia na kumalizika jana jijini Dar es Salaam.  Jumla ya watoto 29 wamefanyiwa upasuaji wa moyo

Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmad akimpatia cheti mtaalamu wa afya kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Center cha nchini Saud Arabia Amani Alqahtani wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha kambi maalumu ya upasuajia wa moyo kwa watoto iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha King Salman na kumalizika jana jijini Dar es Salaam.  Jumla ya watoto 29 wamefanyiwa upasuaji wa moyo


Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akimpatia cheti mtaalamu kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Center cha nchini Saud Arabia wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha kambi maalumu ya upasuajia wa moyo kwa watoto iliyokuwa ikifanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha King Salman na kumalizika jana jijini Dar es Salaam.  Jumla ya watoto 29 wamefanyiwa upasuaji wa moyo

: Baadhi ya wataalam wa afya kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Center cha nchini Saud Arabia wakisikiliza wakati wa hafla fupi ya kuhitimisha kambi maalumu ya upasuajia wa moyo kwa watoto iliyomalizika jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JCKI) jijini Dar es Salaam. Jumla ya watoto 29 wamefanyiwa upasuaji wa moyo.

Picha Na JKCI
************************************************************************************************************************************************************************

Wataalamu wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief kutoka nchini Saudi Arabia wamewafanyia upasuaji wa moyo watoto 29 wenye magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nao.

Upasuaji huo umefanyika ndani ya siku sita na uliwahusisha watoto wenye magonjwa mbalimbali yakiwemo matundu kwenye moyo hitilafu za mishipa mikubwa ya damu, pamoja na matatizo ya valvu za moyo.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha kambi hiyo Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu alisema ushirikiano kati ya JKCI na Saudi Arabia umedumu kwa zaidi ya miaka saba ambapo timu hiyo imekuwa ikifika nchini tangu mwaka 2019.

Dkt. Shemu alisema kambi hizo zimekuwa na manufaa makubwa kwa watoto wanaohitaji matibabu ya moyo pamoja na wataalamu wa ndani kutokana na upatikanaji wa utaalamu na mafunzo ya vitendo kutoka kwa wataalamu mbalimbali wa kimataifa.

“Toka wataalamu wa King Salman Humanitarian Aid and Relief wameanza kufanya kambi za matibabu mwaka 2019 hapa JKCI wameshafanya upasuaji wa moyo kwa watoto wengi uliogharimu takriban shilingi bilioni 6 za Kitanzania. Hiyo ni pesa kubwa sana lakini hatupimi upendo wao kwa pesa hizo tu wamekuwa wakitoa utaalamu wao na kuwafundisha wataalamu wetu wa ndani”, alisema Dkt. Shemu.

Kwa upande wake daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Felix Shonyela alisema watoto waliofanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi hiyo walikuwa na changamoto tofauti zilizohitaji utaalamu wa hali ya juu katika matibabu ya moyo.

“Katika kambi hii tumewafanyia upasuaji wa moyo watoto waliokuwa na matatizo ya matundu kwenye moyo, mishipa ya damu inayoenda kwenye mapafu ambayo haijakaa vizuri na wengine mishipa mikubwa imetoka kwenye vyumba visivyostahili”, alisema Dkt. Shonyela.

Akiwapongeza madaktari hao Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmed Okeish alisema kambi hiyo ni sehemu ya ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika kuboresha huduma za matibabu bingwa ya moyo nchini.

Mhe. Yahya alisema kambi za upasuaji wa moyo kwa watoto zinazofanywa na wataalamu kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa misaada ya kibinadamu wa Ufalme wa Saudi Arabia unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali duniani.

Naye daktari bingwa mshauri wa magonjwa ya moy kutoka Kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Centre cha nchini Saud Arabia Aljohara Mahmoud Hamzah alisema wanafurahi kuona namna ambavyo wanasaidia watoto wa kitanzania kupata huduma katika mazingira ya nyumbani ndio maana wamekuwa wakifika mara kwa mara katika Taasisi hiyo kutoa huduma bingwa za upasauji wa moyo.

“Tunaishukuru timu ya wataalamu wa JKCI kwa kuwa na moyo wa kutukaribisha na kushirikiana nasi kwa pamoja kuokoa maisha ya watoto hawa kwani bila ushirikiano mzuri tusingeweza kutoa huduma kwa watoto wote tuliowapa huduma”, alisema Dkt. Aljohara

 

-         Mwisho -

 




 

Comments

Popular posts from this blog

Serikali yazindua kitabu safari ya upandikizaji wa moyo Tanzania, JKCI yaweka historia mpya ya huduma za kibobezi

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma