JKCI yawa kimbilio la wakazi wa Mwanza, wamiminika kupima moyo
Mbunge wa jimbo la Nyamagana
Mhe. John Nzilanyingi akizungumza na Daktari bingwa
wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Hospitali ya JKCI Dar
Group Mlagwa Yango alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa kambi maalumu
ya matibabu ya magonjwa ya binadamu iliyoandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa
Nyamagana Mhe. John Nzilanyingi kwa ushirikiano na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa
Mwanza katika uwanja wa Nyamagana uliopo jijini Mwanza.
Daktari wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete JKCI Omari Hemedi akizungumza na mwananchi aliyefika katika banda la JKCI kwaajili ya kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya magonjwa ya binadamu iliyoandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Nyamagana Mhe. John Nzilanyingi kwa ushirikiano na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa Mwanza inayofanyika katika uwanja wa Nyamagana uliopo jijini Mwanza.
Fundi sanifu
wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Daffa Suleiman akimpima kipimo
cha kuangalia jinsi mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi
(Electrocardiography – ECG) mkazi wa Mwanza aliyefika katika banda la JKCI
kwaajili ya kufanya uchunguzi wa afya wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya
magonjwa ya binadamu iliyoandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Nyamagana Mhe. John
Nzilanyingi kwa ushirikiano na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
inayofanyika katika uwanja wa Nyamagana uliopo Jijini Mwanza.
Huduma zinazotolewa na
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zimedhihirisha kuwa na uhitaji mkubwa kwa
wananchi katika kile mkoa ambapo taasisi hiyo imekuwa ikifanya kambi maalumu za
matibabu.
Hayo yamesemwa na Mbunge
wa jimbo la Nyamagana Mhe. John Nzilanyingi alipotembelea banda la Taasisi hiyo
wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya
binadamu inayofanyika katika viwanja vya Nyamagana vilivyopo jijini Mwanza.
Mhe. Nzilanyingi alisema
kambi hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Nyamagana kwa kushirikiana na
Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeonesha namna ambavyo wananchi wa
Mwanza wana imani na huduma zinazotolewa na JKCI kwa kuonesha uhitaji mkubwa wa
kutaka kupima moyo.
“Naipongeza JKCI kwa kazi
nzuri inayofanya ya kuwahudumia wananchi wa kila hali, foleni tunayoiona hapa
ikisubiri kupata huduma katika banda la JKCI ni ishara ya imani ya wananchi
waliyonayo kwa taasisi hii kutokana na huduma bora wanayoitoa”, alisema Mhe.
Nzilanyingi.
Kwa upande wake mwananchi
aliyepata huduma katika banda la JKCI aliishukuru Serikali ya awamu ya sita
inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwachagua viongozi wanaojali
wananchi na kuwapa fursa ya kuchunguza afya zao bila malipo karibu na maeneo
wanayoishi.
Salma Mbusu mkazi wa
Mwanza alisema uwepo wa JKCI katika kambi hiyo kumwemwezesha kupima moyo wake,
kuyafahamu vizuri magonjwa ya moyo na kuanza kuchukua hatua dhidi ya magonjwa
hayo.
“Ninamshukuru Mungu kwa
kupata huduma ya kuchunguza moyo wangu nilikuwa na matatizo ya muda mrefu
lakini leo nimepata nafasi ya kupima na kufahamu hali yangu ya afya.
Nimehudumiwa vizuri na kila kitu kimeenda vizuri”, alisema Salma.
Kambi hiyo maalumu ya
matibabu ya magonjwa ya binadamu inayofanyika mkoani Mwanza ni sehemu ya juhudi
za Serikali katika kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi, kuongeza
uelewa kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na kuhamasisha jamii kufanya uchunguzi wa
afya mara kwa mara ili kubaini mapema matatizo yanayoweza kuathiri afya zao.
-
Mwisho -
Comments
Post a Comment