Wananchi wameshauriwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kuwa na bima ya afya ambayo itawasaidia pindi watakapouguwa
Wataalamu wa magonjwa wa moyo wakiangalia maendeleo ya aliyekuwa Mbunge wa Nzega Mhe. Lucas Lumambo Selelii aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rosemary Mpella akimpima shinikizo la damu mwilini (BP) aliyekuwa Mbunge wa Nzega Mhe. Lucas Lumambo Selelii aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Wananchi wameshauriwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwa kufanya hivyo watatambua kama wana maradhi au la na kama wana maradhi wataweza kupata huduma za matibabu kwa wakati. Pia wameombwa kuwa na bima ya afya ambazo zitawasaidia kupata matibabu pindi watakapouguwa kwani maradhi huja muda wowote, wakati wowote na mahala popote bila ya kupiga hodi. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na aliyekuwa Mbunge wa Nzega Mhe. L...