Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Pedro Pallangyo akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) Bernard Konga mwitikio wa wananchi kufanya uchunguzi wa afya ya
mioyo yao katika banda la JKCI wakati wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam.
Huduma
mpya kabisa ya kutibu tatizo la mfumo wa umeme ulioharibika kwa njia ya kisasa
zaidi inatarajiwa kuanza kutolewa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),
kati ya kipindi cha kuanzia mwezi Agosti hadi Oktoba, mwaka huu.
JKCI
hivi sasa ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ili kuanza kutoa huduma hiyo
baada ya kupatiwa na Serikali kiasi cha Sh. bil 4.3 kwa ajili ya kusimika
mitambo pamoja na kuanzisha chumba kingine cha tatu cha upasuaji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi aliweka wazi hayo hivi karibuni
alipozungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Maonesho ya 44 ya
Biashara ya Kimataifa (SABASABA) ambako JKCI inashiriki kutoa huduma ya
uchunguzi wa awali wa magonjwa ya moyo pamoja na elimu kwa wananchi jinsi ya
kuepukana na magonjwa hayo.
“Maandalizi
yanakwenda vizuri, tunatarajia kati ya Agosti hadi Oktoba, mwaka huu, pale JKCI
tutaanzisha huduma mpya kabisa, mfumo wa umeme unapoharibika tutakuwa tunaweza
kuingia ndani ya moyo, tukatizama sehemu zilizoathirika na kuziunguza ama
kuzifanyia marekebisho,”
“Huduma
hiyo kitaalamu inaitwa ‘Electrophysiology studies’ ni huduma ambayo haijawahi
kutolewa hapa nchini na maandalizi ya kuanzisha chumba cha tatu cha upasuaji
nayo yanakwenda vyema” alisema Prof. Janabi.
Aliongeza
“Hapa SABASABA hii ni mara ya nne JKCI tunashiriki, mwaka jana tulipata zawadi
ya kuwa banda lililotoa huduma bora kwa upande wa huduma za afya SABASABA.
“Mwaka
jana banda letu lilikuwa dogo, mwaka huu tumeongeza karibu mara mbili na nusu,
tangu tumeanza hadi sasa namba ya watu tulioona imeongezeka. Tumeona zaidi ya
watu 1,000 na takribani watu 370 tumewakuta na Shinikizo la Juu la Damu na
walikuwa hawajijui hali zao hapo kabla.
“Tumewapa
rufaa kuja kwenye taasisi yetu kwa matibabu zaidi, katika banda letu tunavyo
vifaa ikiwamo kipimo cha Electoral Cardiograph (ECG), tunao madaktari wa
chakula kwa wanaohitajika kupunguza uzito, wanapewa elimu.
“Yupo
daktari wa nasaha anatoa elimu kwanini mtu asiache kunywa dawa na pale zinapomsumbua
nini cha kufanya, tunao madakrari bingwa wa udhamiri wa magonjwa ya moyo
nikiwamo mimi mwenyewe.
“Tunaonesha
pia vifaa kadhaa vinavyotumika wakati wa upasuaji, tunavyo vile tunavyotumia
kusimamisha moyo pale inapohitajika kufanya marekebisho wakati tunafanya
upasuaji,” alisema Prof. Janabi.
Aliongeza
“Tunajaribu kuwaeleza wananchi waelewe, pia tulipata mgonjwa mmoja hapa
Sabasaba ambaye amehangaika kutafuta matibabu, tulipompima kipimo cha Echo
Cardiograph (ECHO) tuligundua moyo wake unafanya kazi chini ya kiwango cha
asilimia 30.
“Ikiwa
tusingemgundua hapa maana yake angeendelea kuhangaika na kutumia fedha nyingi
kujitibu, kutokana na hali yale pale JKCI tunacho kifaa kinachoitwa CRTD
ambacho tunaweza kumpandikiza na akaimarika afya yake na kuendelea na maisha
yake kama kawaida,” alisema.
Alisema
bila kupepesa maneno JKCI imekuwa na mchango mkubwa kwenye tiba ya magonjwa ya
moyo ndani ya nchi na katika nchi jirani zinazotuzunguka.
“Zanzibar,
Malawi, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wote hawa huduma kama
zetu hawana, tunawahudumia hapa JKCI.
“Rwanda
tulipeleka timu yetu mbayo ilikaa wiki nzima na kafanya upasuaji kwa wagonjwa
25, hii yote tunaishukuru Serikali kwa sababu imekua pamoja nasi katika kila
hatua ya kuimarisha huduma za matibabu ya moyo hapa nchini,” alisisitiza.
Comments
Post a Comment