TAARIFA KWA UMMA
TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI WAKATI WA MAONESHO YA SABASABA
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kuwa inashiriki maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Biashara wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 01/07/2020 hadi tarehe 13/07/2020.
Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na mikoa ya jirani mnakaribishwa kutembelea Banda letu lililopo ukumbi wa Karume  ili muweze kupata huduma mbalimbali zinazohusiana na afya ya Moyo.
Madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo chini ya uongozi wa Prof. Mohamed Janabi watakuwepo  katika banda letu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi. 

“Tunajali Afya yako”.

 Imetolewa na:



Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
01/07/2020

Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI kutanua huduma za matibabu ya moyo nchini