Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane akimkabidhi cheti cha pongezi mstaafu ambaye alikuwa Afisa Uuguzi wa JKCI Marcelina Granima wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu iliyofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Na: JKCI Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufanya kazi kwa uweledi, ufanisi na kuepuka vitendo vyote vinavyoweza kuwasababishia kushindwa kufikia hatua ya kustaafu katika utumishi wa umma. Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tatizo Waane wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu wawili waliofikia ukomo wa utumishi wa umma hivi karibuni na kuagwa leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa hafla hiyo Dkt. Waane amesema kuwa wapo watu wengi ambao wanaanza utumishi wa umma katika ngazi mbalimbali lakini hawafikii ukomo wa utumishi wao kutokana na sababu mbalimbali, hivyo ni vyema kwa...