CRDB MARATHON YACHANGIA MILIONI 200 KWA AJILI YA MATIBABU YA WATOTO 100 WENYE MAGONJWA YA MOYO WANAOTIBIWA JKCI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwaongoza viongozi wengine katika matembezi ya kilometa 5 wakati wa mbio za CRDB Marathon kuchangia matibabu ya watoto 100 wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI leo Jijini Dar es Salaam 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akirishiki mazoezi ya viungo mara maada ya kumalizika kwa mbio za CRDB Marathon zilizofanyika katika Viwanja vya Farasi Oyster bay leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchangia watoto 100 wenye magonjwa ya Moyo wanaotibiwa JKCI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza wakati wa mbio za CRDB Marathon kuchangia watoto 100 wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI zilizofanyika katika Viwanja vya Oyster bay leo Jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi hundi ya shilingi milioni 200 iliyotolewa leo katika Viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB zilizokusanywa kutoka kwa washiriki wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto 100 wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI. Hii ni mara ya pili kwa Benki hiyo kuratibu mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walioshiriki mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchagia watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mbio hizo zilizofanyika katika Viwanja vya Farasi Oyster bay leo Jijini Dar es Salaam


Picha na: JKCI

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari