JKCI yafikisha elimu ya chanjo ya UVIKO – 19 kwa Wafanyakazi wa TICTS
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joshua Ogutu akimchoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 mfanyakazi wa Tanzania International Container Terminal Services – TICTS Jana katika ofisi za TICTS zilizopo Kurasini Jijini Dar es Salaam
Na: JKCI
Wafanyakazi
wa kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services – TICTS
wameishukuru Serikali ya awamu ya sita pamoja na watendaji wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuwathamini na kuwafuata maala pa kazi kwa ajili ya
kutoa chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19
Wakizungumza
wakati wa zoezi la kutoa chanjo ya UVIKO – 19 lililofanyika Jana katika ofisi
za TICTS zilizopo Kurasini Jijini Dar es Salaam wafanyakazi hao wamesema kuwa
kutokana na ratiba ngumu waliyonayo katika kutekeleza majukumu yao ingekuwa
ngumu kwao kupata elimu sahihi ya chanjo ya UVIKO -19 pamoja na kupata chanjo
kama wataalam kutoka JKCI wakiongozwa na Prof. Mohamed Janabi wasingefika
katika eneo lao la kazi na kuwapatia fursa ya kuchanja chanjo hiyo kwa hiari.
Akizungumza
na waandishi wa habari, mfanyakazi wa TICTS Rose Kalima amesema kuwa baada ya
kupata hamasa kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan kwa hiari yake alitamani kupata chanjo ya kuzuia maambukizi ya
UVIKO – 19 lakini kutokana na ratiba za kazi kumbana hakuweza kwenda kuchanja
hadi wataalam wa JKCI walipofika katika ofisi za TICTS.
“Nimefurahi
leo nimepata chanjo ya UVIKO – 19 kwa urahisi bila ya kuangaika kwenda
kuitafuta, elimu tuliyoipata leo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof.
Janabi pia imetupa hamasa kubwa kujitokeza mbele kuchanja, Wito wangu kwa
wanawake waache kusikiliza maneno ya mtaani yanayopotosha kuusu chanjo,
ingekuwa na madhara kama ambavyo tunadanganyana mtaani wataalamu wangetuambia
maana sisi ndio mama na dada zao hivyo sidhani kama mtu angeweza kumuangamiza
mama ama dada yake” alisema Rose.
Kwa
upande wake Revokatus Deus ambaye pia ni mfanyakazi wa TICTS ameushukuru
uongozi wa TICTS pamoja na JKCI kwa kuwapa wafanyakazi wa TICTS nafasi ya pekee
kupata elimu inayoonyesha faida nyingi za kuchanja chanjo kuzuia maambukizi ya
UVIKO – 19.
“Sikutegemea
kama ipo siku hata sisi huku tungefikiwa na wataalamu hawa kutupa elimu
inayoweza kumbadilisha mtu kutoka katika mawazo hasi na kuwa balozi mzuri
katika jamii inayonizunguka, nimepata elimu sahihi ya chanjo ya UVIKO – 19,
faida ni nyingi zaidi kuliko hasara, watanzania endeleeni kuchanja chanjo kwani
afya yako ni mtaji wako” alisema Revokatus
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania International Container Terminal Services –
TICTS Hui Horace amewataka wafanyakazi wa TICTS kuendelea kuchukua taadhari
zilizowekwa na Serikali dhidi ya ugonjwa wa UVIKO – 19 ikiwemo kuvaa barakoa,
kunawa mikono na maji safi na tiririka, pamoja na kuchanja kwa hiari ili kuweza
kuwakinga wengine pamoja na kuwa na afya bora.
“Mimi
pia ni muhanga wa ugonjwa wa UVIKO – 19, ndio maana najilinda na kuwalinda nyie
kwani mna wajibu katika familia zenu hivyo jilindeni ili familia zenu ziendelee
kuwa na furaha” alimema Hui
Comments
Post a Comment