Wachezaji wa Mpira wa Miguu kutoka Klabu za Yanga, Simba, Azam na Simba Queens wachoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO - 19

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa elimu kuhusu chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 kabla ya chanjo hiyo kuanza kutolewa kwa wachezaji wa klabu za Yanga, Simba na Azam.



Baadhi ya wachezaji wa mpira wa miguu kutoka klabu ya Simba wakifuatilia elimu kuhusu chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 iliyokua ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kabla ya chanjo hiyo kuanza kutolewa kwa wachezaji hao leo Jijini Dar es Salaam.


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Oliver Marandu akimchoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 mchezaji wa mpira wa miguu kutoka klabu ya Yanga Abdallah Shaibu (Ninja) baada ya wachezaji wa klabu hiyo kufika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuchoma chanjo


Mchezaji wa mpira wa miguu kutoka klabu ya Simba Queens Aisha Juma akichoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Oliver Marandu akimchoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 mchezaji wa mpira wa miguu kutoka klabu ya Azam Nicolaus Wadada baada ya wachezaji wa klabu hiyo kufika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuchoma chanjo

Mchezaji wa mpira wa miguu kutoka klabu ya Simba Rally Bwalya akichoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)


 

Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI, MOI NA MNH waitwa Comoro kutoa huduma za matibabu ya kibingwa