Viongozi wa Serikali, wananchi pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wachoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19


 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea umuhimu wa kuchanja  chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 kabla ya chanjo hiyo kuanza kutolewa kwa viongozi wa Serikali, wananchi pamoja na wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Afisa  Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joshua Ogutu akiandaa sindano yenye  chanjo ya  kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 kwa ajili ya kumchoma mwananchi aliyefika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuchoma chanjo hiyo.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Gudila Swai  akimchoma chanjo ya kuzuia maambukizia ya UVIKO – 19 Balozi mstaafu Modest Mero aliyefika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuchanjwa chanjo.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rydness Mlashani akimkabidhi cheti  cha uthibitisho wa chanjo balozi mstaafu mara baada ya kuchoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 inayotolewa  katika Taasisi hiyo  iliyopo jijini Dar es Salaam. 


Mkurugenzi wa Kurugenzi  ya  Uuguzi ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimkabidhi cheti cha uthibitisho  pamoja na fomu ya kukubali kuchoma  chanjo  ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa JKCI CPA Agnes Kuhenga mara baada ya kuchoma chanjo hiyo.

Afisa Uuguzi  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joshua Ogutu akimchoma mkazi wa jijini Dar es Salaam  chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO -19.


Afisa Uuguzi  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Oliver Marandu akimwelezea mwananchi umuhimu wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO -19 aliyoichoma katika Taasisi hiyo.



Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari