Viongozi wa Serikali, Wafanyakazi wa sekta ya Afya na Wananchi waendelea kuchomwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO -19 inayotolewa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Balozi Mteule Togolani Mavura akichanjwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya
UVIKO – 19 inayotolewa katika Taasisi ya Moyo Jakaya ikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.
Mohamed Janabi akielezea umuhimu wa kuchanja chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19
kabla ya chanjo hiyo kuanza kutolewa kwa viongozi wa Serikali, wananchi pamoja
na wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Kurugenzi
ya Uuguzi ya Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akitoa maelekezo ya namna
watakavyochanja chanjo ya kuzuia
maambukizi ya UVIKO – 19 kwa wananchi waliokuwa wanasubiri kuchanja chanjo hiyo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho akichomwa
chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO -19
katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Afisa Uuguzi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joshua Ogutu akimchoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19 mwananchi
aliyefika JKCI kwa ajili ya kuchoma chanjo hiyo.
Afisa Uuguzi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Oliver Marandu akimchoma chanjo ya kuzuia
maambukizi ya UVIKO -19 mwananchi aliyefika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuchoma chanjo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Joshua Ogutu akiandaa sindano yenye
chanjo ya kuzuia maambukizi ya
UVIKO – 19 kwa ajili ya kumchoma mfanyakazi wa Taasisi hiyo.
Mwananchi akimuuliza swali Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
kama mama anayenyonyesha anaweza
kuchomwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya
UVIKO – 19.
Mkazi wa jijini Dar es Salaam akimuuliza swali Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi kama mgonjwa wa kansa anaweza kuchomwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO – 19.
Afisa Uuguzi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Msabila akiwaandikia wananchi vyeti vya
uthibitisho wa chanjo mara baada ya kuchomwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya
UVIKO – 19 inayotolewa katika Taasisi
hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Oliver Marandu akitoa maelekezo kabla ya
kuwachoma chanjo ya kuzuia maambukizi ya UVIKO -19 wananchi waliofika katika
Taasisi hiyo kwa ajili ya kuchoma chanjo.
Comments
Post a Comment